Pale jijini Liverpool Kuna mkosi gani!? hasa team ya Liver!!? Je, ni hujuma!!?

Pale jijini Liverpool Kuna mkosi gani!? hasa team ya Liver!!? Je, ni hujuma!!?

RESILIENT KATO

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2024
Posts
4,504
Reaction score
8,842
Miaka ya zamani kidogo hasa 1988/1989 kulitokea janga uwanjani na kuua mashabiki wengi sana Hillsborough disaster, Liverpool wakafungiwa kucheza michuano ya ulaya kwa miaka mingi sana!Hadi Leo Kuna kesi mahakamani ya kupinga mashabiki kuhusika kwenye fujo zilizozaa janga hilo,mwaka 2020 baada ya Liverpool kutwaa ubingwa kesi ilisikilizwa na Bado mashabiki wakaonekana ni wao ndio wa kualumiwa na sio maafisa wa polisi!wanazi wa Liverpool wakapinga Kwa kusema "justice denied"

Juzi baada ya Liverpool kutwa taji na shangwe kurindima jijini,Jana kwenye parade katokea MTU na gari lake kaenda kugonga maksudi kabisa mashabiki na kuwajeruhi watu takriban 47,Hadi Sasa hivi insemekana shangwe na parade la ushindi vitaahirishwa kutokana na madhila hayo,Sasa tujiulize kwanini haya mambo hutokea kwenye Jiji la Liverpool hasa inapotokea mechi au shangwe za michezo zinapotokea!!?

He Liverpool kama team na Jiji lake wanahujumiwa!!?

Kumbuka Liverpool ndio Jiji pekee lenye magofu na majengo ya kizamani sana halina majengo ya kisasa na inaonekana ni jiji lililotelekezwa Sana na ndio maana Hadi leo wanazomea wimbo wa taifa wa uingereza!!

Na Mimi kama mshabiki kindaki ndaki wa timu hii nimefuatilia kwa kina nikagundua hasa kwenye mechi nyingi hasa enzi za Ferguson Tim ilihujumiwa na marefa uwanjani mara nyingi sana Hadi Rafael Benitez akalalama sana!!Hats jurgen klopp amekua akilalamikia waamuzi kwa muda mrefu!!

Kuna jambo pale Liverpool nadhani figisu hazipo huku kwetu tu,hata ulaya zipo!!

You'll never walk alone!
 
Back
Top Bottom