Pale kaka yake alipo dhamiria kumuua mdogo wake kisa mdogo wake kaondoa Ng'ombe zake kwa kaka yake

Pale kaka yake alipo dhamiria kumuua mdogo wake kisa mdogo wake kaondoa Ng'ombe zake kwa kaka yake

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
6,944
Reaction score
14,351
Huenda Heading isilete maana ya moja kwa kwa moja lakini kwenye maelezo nitaeleza kwa kirefu sana.Japo ni ndefu ila nitafupiza sana mimi sijui kuandika ....".inaendelea"

Hii ni familia kubwa ya kisukuma ambayo baba yao mzazi alifariki miaka zaidi ya 30 iliyopita.Hivyo kwa utamaduni wa kisukuma kijana mkubwa wa kiume ndo hurithi uongozi wa familia na kuwa kama baba.

Hata kama mama atakuwepo lakini maamzi ya mwisho yatatoka kwa kaka mkubwa wa familia sijui makabila mengine kwao ikoje.

Familia hii ni majirani na ndugu pia wao ni watoto wa shangazi yetu kiukoo yaani sio wa toka nitoke na baba yetu la! hivyo tumechunga nao sisi tukiwa watoto wadogo na kazi yetu kipindi hicho ilikuwa kuangalia mifugo wao wanazama porini kuwinda nk.

Baada ya kuamua kugawana ng'ombe za urithi kama ilivyo kawaida wengine waliuza na kumaliza kabisa hadi mashamba pia waliuza.Ikumbukwe wamegawana mama yao akiwa yu hai bado na amefariki mwaka 2019 tu.

Hiki kisa kitawahusu watu wa3 tu wahusika japo ilikuwa ni familia ya watu zaidi ya 9 me na ke.
Kaka mkubwa nitamuita Maneno na aliyepeleka ng'ombe kwa kaka yake nitamuita Bahati halafu mdogo wao kati yao wote nitamuita Yatabu.

Basi baada ya wenzao kuuza ng'ombe hawa watatu ndo walibaki nazo japo hawa wawili yaani Bahati na Yatabu waikuwa nazo chache tu zilizo baki makisio kama ng'ombe 3-5 kwa kila mmoja ijapokuwa kaka yao mkubwa Maneno alikuwa nazo nyingi sana kama 40-50.

Maneno alikuwa mtu mwenye ushawishi kijijini hivyo alijiingiza kwenye siasa na hatimae kugombea udiwani na kushindwa kwa mara mbili mfurulizo.Hii ilimfanya ashuke sana kiuchumi maana alikuwa anategemea mifugo na kilimo na alikuwa mkulima mwenye kuheshimiwa pale kijijini.

Siasa ilishusha kwa kasi sana uchumi wake hadi akaanza kukopa na kukodisha baadhi ya mbuga na hadi kuuza kabisa mbuga zilikuwa zinampa magunia mamia ya mpunga.

Ng'ombe kutoka kwenye 50 zikapungua hadi 17 hivi.Muda huo huyo Bahati ukwasi ukamea kwa kasi sana kwani alikuwa anafanya biashara ya duka pamoja na kulima.Hivyo alipoona kaka yake mkubwa uchumi umeanguka na isiwe aibu kwakwe na familia basi akaanza kununua Ng'ombe minadani na kumbuka mnada mmoja wa kamena (upo geita)alinunua ng'ombe zaidi ya 17 na kuwapeleka kwa kaka yake ili heshima iendelee kuwepo.

Kumbuka na zile ng'ombe zake za urithi zilikuwepo palepale kwa kaka yake (Maneno) hivyo ghafla zizi likaanza kujaa ndani ya miezi michache tu ng'ombe walizidi idadi ya 50 na heshima ikarudi upya tena kijijini.

Wengi wa watu walijua jamaa kanyanyuka tena kwa kasi lakini wachache wetu ndo tulikuwa tunajua kuwa ng'ombe ni wa mdogo wake hizi ikiwa mimi ni mmoja tulioenda kuchagua hao ng'ombe kamena mnadani.


Basi kaka yake huyu(Maneno) wivu ukamjaa akaanza kuuza ng'ombe wa mdogo wake na kutoa taarifa ng'ombe wameibwa na kwa sababu Bahati hakuwa na wasiwasi na kaka yake mkubwa aliamini.Idadi ya ng'ombe za kuibwa kama alivyokuwa anaambiwa na kaka yake zikafika hadi7!!

Basi siku moja Maneno alishilikiana na mchungaji wake kuiba kumbe lengo lake iwe ushahidi kuwa mchungaji ndo huwa anaiba ng'ombe zile.....yule mchungaji alichukua ng'ombe wa makamo muda wa saa5 usiku kama alivyoambiwa na boss wake ampeleke mahali fulani atakuta wanunuzi wakiwa tyr yeye arudi na hela tu.

Akiwa njiani huyu mchungaji wa kirundi ghafla walitokea jamaa 2 wakiwa na baiskeli kisha wakaanza kumuhoji unaipeleka wapi hii ng'ombe usiku huu? kumbuka kijana huyu alikuwa anamswaga yule ng'ombe kwenye njia isiyo rasmi ...Baada ya kijana kujitetea alikubali kuwa Boss wake apigiwe simu kabla ya yowe kupigwa.

Bwana maneno akapokea ile simu kisha akamulu mleteni ofisi ya sungusungu ......baada ya kufika muda uleule alipigwa viboko sana yule dogo kadiri alivyokuwa kuwa anasema boss ndo alikuwa amepanga waibe ndivyo viboko vilizidi kurindima kwa mchungaji yule maana watu walikuwa wanaamini wale ng'ombe ni wa maneno hivyo haikuwa rahisi yeye boss ajiibe.

Baada ya muda Maneno aliamru aachwe kupigwa na yeye atalimaliza kwa kuwa ng'ombe kapatikana.
Kweli lile sakata liliisha kimya kimya huku Bahati akizidi kumuamini kaka yake kuwa ni kweli zile ripot alikuwa anampa za wizi ni za kweli.

Ukisikia Mungu hamtupi mja wake au za mwizi ni arobaini basi ndo hizi

Basi siku moja huyu Bahati akiwa viunga vya mnadani aliona wale Ng'ombe wake wamekuja kuuzwa na mtu
japo hakuwa na uhakika nao sana kama ndo wenyewe basi hapohapo mnadani alimtafuta mtu aliyehusika kuwa swaga kuwatoa kamena hadi kwa Maneno na kwa sababu yule mswagaji ndo kazi yake na ni maarufu wala hakuchukua muda akampata.

Akamwambia nimewaona wale ng'ombe wangu wapo hapa mnadani nenda nawewe ukahakiki halafu tujue cha kufanya ......jamaa aliwaangalia mara moja tu akasema ndo wenyewe kabisa kabisa.Hivyo likaanza yowe la kimya kimya hapo hapo mnadani(huu mnada sitautaja).

Hatimae wale wauzaji wakazingirwa pale pale yowe la sauti likaanza wiziwizi sime,fimbo,mawe waakanza kurushwa wale watu wakiitwa wezi.Bahati nzuri police huwa wako palepale wakawaokoa ....na baada ya kuwaokoa moja kwa moja kituoni na huyu aliyedai kuwa hawa ng'ombe ni wake yaani Bahati.

Wale jamaa walioshutumiwa kuwa ni wezi walisema kweli yote kuwa "Hawa ng'ombe 4 tulinunua kwa Maneno wa kijiji X kwa makubaliano ya kuja kuwachinja maana sisi kazi yetu ni bucha baada ya kuwafikisha nyumbani hawa ng'ombe tuliwapenda na kutulazimu tuwafuge na mwingine yule wa4 amezaa yupo nyumbani tumemuacha lakini hawa imetubidi tuuze kwa sababu soko lipo vizuri kwa sasa"

Bahati aliishiwa nguvu akajikaza kwanza akampigia simu kaka yake Mneno ambae kwa muda huo tyr alikuwa ameambiwa nini imejiri mnadani kuwa wale ng'ombe wake walio ibwa leo wamepatikana.Baada ya kupokea tarifa zile bw maneno alizima simu na kuondoka nyumbani bila kuaga hadi kahama .......


Bahati alipotoka police siku hiyhiyo aliwapa watu hela wakatengeneza zizi kwa mdogo wake Yatabu kama unakumbuka nimemtaja huko juu. Yatabu alikubali kwa moyo mmoja maana alikuwa haishi mbali na kaka yao Maneno na kipindi hicho yeye ng'ombe wake anao hapohapo kwakwe alikuwa na ng'ombe 6 tu.

Basi zizi lilijengwa kwa speed hadi jioni limekamilika na ng'ombe walipotoka marishoni tu hapohapo walitenganishwa Bahati akiwa na mama yake na wadogo zake na majirani walishuhudia akibagua ng'ombe wake na kuwapeleka kwenye zizi jipya kwa Yatabu pamoja na mchungaji wake alihama siku hiyohiyo.

Maneno alibakiwa na ng'ombe wake halali 9 tu ikiwa pamoja na ndama.Kumbuka ng'ombe wamechukuliwa akiwa kakimbia japo mama yao mzazi aliwasihi sana walimalize kifamilia hata kuhusu kule police likaisha na jamaa wale walinunua bila kibali pia nao walipata stahiki yao kutoka kwa police.

Basi maneno pamoja na kufanya madhambi hayo yote bado aliona kaaibishwa sana na mdogo wake hasa kuondoa wale ng'ombe kwake na kuwapeleka ghafla kwa mdogo wao aliumia mno mno hadi alikonda .

Alikuwa anauza maziwa sasa hauzi tena hata mbolea hatapata tena ile heshima ya kuwa ana ng'ombe wengi hana tena hata yale majembe ya kukokotwa na ng'ombe (pirao) hana tena yaani akihitaji akalimiwe atoe hela au akaombe kwa mdogo wake!je ataanza vipi kuomba sasa na tyr iko wazi kama mbuzi yeye ndo alikuwa anaiba wale ng'ombe?

Alibaki na maswali mengi sana na jibu lililokuja basi ammalize kabisa mdogo wake hakuna namna nyingine.

Kulikuwa na sherehe kubwa pale kijijini Bahati nae alikuwa mtu muhimu sana hivyo hakukosa siku ile na siku ile kaka yake Maneno naye alikuwa amediriki atimize ubaya na alifanikiwa kwa kumwekea dawa kwenye kinywaji akitumia chawa wake au mashushu wake.

Baada ya siku chache jamaa alianza kukohoa vibaya mno wakampeleka kamanga,bugando,waja,agakhan bila bila ugonjwa hauonekani na hali inazidi kuw mbaya.Bahati hatimae hata kuongea akawa hawezi na msaada mkubwa anaoutegemea ni kutoka kwa mdogo wake yatabu, dada zake pamoja na mke wake walio zaa nae watoto 6 na mkubwa ni wakike kamaliza kidato cha4 mwaka jana.

Kwa sababu wameenda hospital kubwa bilabila chaguo la mwisho ni kwenda kwa mganga wa kienyeji.
Yule mganga alimwambia ng'ombe zako ndizo ndo chanzo cha haya yote!.Basi aliendelea kupata huduma kwa mganga akiwa haongei hivyohivyo ila hali yake ilizidi kupata matumaini.

Amekaa kwa mganga kwa miaka3 na mwezi wa1 mwaka huu amerudi kwake akiwa imara na kwa sababu mke wake alilishikiria duka vizuri na kumtibia mme wake kwa miaka yote ile alikuwa karibu naye akimpa matumaini mmewe.Basi aliporudi na kukuta duka bado lipo tena limeongezeka zaidi jamaa kamwambia mke wake wee endelea na duka na mimi niende machimboni. Yuko huko Machimboni kanunua karasha 2 kuhusua hela aliko toa mimi sijui.

Ni leo tu nimeongea nae mimi mwenyewe kwa simu na kuniambia hilo la mke wake kumwachia duka na yeye kuwa machimboni. Ikumbkwe mwaka 2023 nilifunga safari hadi kwa mganga alipokuwa anapata matibabu nililala kule siku2 kwa mganga nilimuona jamaa hana matumaini kabisa amekonda ngozi imeharibika amekuwa kama mzee macho yameingia ndani kwa kweli hata mimi niliona jamaa hachomoki kidogo tu nimwambie aniachie wosia nirudi nao.

Nikiwa nae pale kwa mganga usiku hata sikumbuki ilikua sangapi Bahati alilia sana kwa sauti akisema nikifa hakikisha wewe (MIMI)na yatabu(mdogo wake ndo alikuwaga nae muda wote kwa mganga) mali zilizopo zitumike kuwasomesha watoto wangu hakikisheni watoto wangu wanasoma tena shule nzuri.

Tulimbembeleza huku mimi nikijua kwisha kabisa huyu jamaangu leo hatoboi nimekuja kufanyaje huku halafu nirudi na maiti? Sikulala kwakweli usiku ule nikajua huyu mdogo wake lazima atajua mimi kuna kitu nimeleta sio bure na mimi nita shutumiwa kumalizia kazi maana mimi na Kaka yao (maneno) tulikuwa marafiki japo mimi ni mdogo sana kwao na urafiki wangu haukuishia kwa kaka yao tu hata wao pia.

Kesho yake niliamka akiwa mzima by saa3 asbh nikaaga nikaondoka nikimwambia nitarudi tena kumuona.
Nilipofika tu sikulala kwangu nikaenda kuwaambia wazazi wangu yote aliyoniambia jamaa maana niliamini muda wowote nitajurishwa lolote litatokea.Imagine mtu anakunywa uji hata kikombe hamalizi lakini mnakuwa mnaona tumboni kitu kigumu kama jiwe kinapanda juu na kushuka na muda huo jamaa analia kwa maumivu makubwa kama mtoto.Niliwaambia na mke wa jamaa nae nikamwambia kwa simu.


MWISHO.

KWENYE HIKI KISA UMEJIFUNZA NINI MDAU ?
 
Back
Top Bottom