Pale kinyesi cha mnyama kinapotengenezwa kupata kinywaji ghali Duniani

Pale kinyesi cha mnyama kinapotengenezwa kupata kinywaji ghali Duniani

Mokaze

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2018
Posts
14,370
Reaction score
14,929
Habari zenu wakuuu.

Huko Indonesia kwa muda sasa wamegundua njia bora ya kuzalisha kahawa bora inayoitwa "Luwak coffee" kupitia kinyesi cha mnyama wanayemuita Luwak au "Civet cat".

Mnyama huyo pamoja na vyakula vingine anapenda kula mbegu mbivu za kahawa (buni), kwakuwa tumbo lake haliwezi kusaga kokwa za buni hivyo hunya hizo kokwa jinsi zilivyo katika mfumo wa "lump" (kiburungutu cha kinyesi) zikiwa tayari zimechachuliwa na kemikali-mmeng'enyo (digestive juices) pale mbegu hizo zilipokuwa tumboni mwa huyo myama, na ni katika hatua hiyo ya mmeng'enyo ndipo hiyo kahawa hupata Ubora wake unaoipa thamani, kwa maneno mengine digestive juices za huyo mnyama huingia katika hizo mbegu na kuzipa flavors kuzifanya ziwe na ladha bora.

Hivyo vibulungutu (mkusanyiko wa mbegu za buni-undigested) au kwa lugha nyepesi kinyesi hukusanywa na kuoshwa kisha kuanikwa na kuingizwa kwenye mchakato wa kutengeneza kahawa kwa ajili ya mauzo, Kilo moja ya buni zitokanazo na kinyesi cha huyo mnyama inakaribia $ 150 au zaidi.

Huyo mnyama Luwak (Civet cat) kwa asili ni mnyama pori na wapo wachache hivyo wakulima wa kahawa huko Indonesia wameamua kufanya mpango wa kuwafuga ili wazaliane kwa wingi ili kukidhi haja ya uzalishaji mkubwa wa "kahawa ya Luwak" hivyo kujiongezea zaidi kipato.

Katika Kuinua zao la kahawa nchini Tz nasi tunaweza kujifunza njia hiyo kupitia Indonesia, swali ni je kwa njia ipi tunaweza kuwapata hao wanyama (civet cats) na je wanaweza kuishi katika mazingira yetu??

Karibuni wadau kwa mjadala.
 
Tz ina takribani kila aina ya maeneo yenye kila aina ya hali ya hewa tofauti tofauti kuweza kufuga hao paka pori utafiti ukifanywa.

Ila sasa, tuwekee picha ya hao viumbe kwanza ili tuwatathimini kabla ya kufanya maamuzi.

Maana unapoamua kula mavi ya kuimbe chochote lazima ujiridhishe kwa kuiona sura yake ilivyokaa kaa kwanza!

Wakurya siyo wajinga kula "kichuri" ambacho ni kinyesi halisi cha ng'ombe.
 
Screenshot_20230205-065449.png
 
Sasa kwanini wanasayansi wasichukue sample wakabaini jinsi ya kutengeneza hiyo kemikali maabara 😀😀😀 au ndo maajabu ya Mungu kwamba kuna vitu binadamu hatuwezi kuvitengeneza kwa maarifa yetu .
 
Back
Top Bottom