Pale mtu wa karibu anapofariki tunaumia, kwanini pia tusifurahi endapo maisha ya marehemu yalikuwa na mateso makali sana na kifo kikaweka tamati?

Pale mtu wa karibu anapofariki tunaumia, kwanini pia tusifurahi endapo maisha ya marehemu yalikuwa na mateso makali sana na kifo kikaweka tamati?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Kiukweli kifo cha mtu wa karibu huwa kinauma sana kwa wafiwa kitu kinachotupelekea hata wanaume wazima kujifungia vyumbani kulia machozi hadi kamasi kwa maumivu jinsi yalivyo.

Tukiachana na upande wa maumivu, kuna muda unakuta marehemu katika maisha yake alikuwa na matatizo yaliyomtesa sana kama magonjwa yenye maumivu makali sana, kwenda jela zenye mateso makali kifungo cha maisha, n.k.... kwa kifo chake ni wazi kabisa sasa marehemu kapumzishwa na mateso aliyokuwa akipitia yaliyotuumiza hata sisi, kwanini kwa upande wa pili isizoeleke kufurahia kifo chake endapo kifo kimestopisha hayo maumivu?
 
Kifo kisikie kwa mwenzako tu.

Haijalishi ana maumivu gani. Ila kuongea ongea nae inaleta amani sana
 
hivi mtu yupo gereza la maweni kule Tanga au ana ugonjwa unaompa maumivu makali sana kila siku mpaka analia, hapo utaongea nae kitu gani.

kuna vitu visikiage tu kwa wengine
Ikiwa mtu bado anaishi bado kuna tumaini bila kujali yupo kwenye situation gani matatizo huwa yanapita tu
Lakini mtu akifa hakuna tena tumaini kuhusu mambo ya duniani
Kifo kinafikirisha sana

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Kinachotuumiza hasa ni imani yetu haba kuwa ndiyo basi tena hatutaweza kuonana na ndugu yetu kipenzi kamwe/milele!

Ila kwa wale wenye imani katika Kristo Yesu huwa tunaumizwa papo kwa hapo kibinadamu ila huwa ni wepesi kuamini ipo siku moja tutakutana na Mpendwa wetu aliyetutoka paradiso sababu Yesu ndiye njia ya ukweli na uzima.

Ikiwa Yesu(njia ya uzima wa milele) aliishinda mauti na ndiye mwokozi wetu basi nasi kwa neema na rehema zake Mungu tutashinda kifo kwa imani thabiti na matendo mema.
 
Unakuta watoto wanakula butter & chicken huko town, hawamjali mzazi wao siku mzazi akifa kwa homa ambayo ingetibika kwa dozi ya 3,500/= mitoto inaenda kupiga kelele msibani
 
Mleta mada u Genius,swali lako linafikirisha sana sana...
 
Maumivu hayavumiliki yanakuja automatically unajikuta unalia
 
Kiulweli kifo cha mtu wa karibu huwa kinauma sana kwa wafiwa kitu kinachotupelekea hata wanaume wazima kujifungia vyumbani kulia machozi hadi kamasi kwa maumivu jinsi yalivyo.

tukiachana na upande wa maumivu, kuna muda unakuta marehemu katika maisha yake alikuwa na matatizo yaliyomtesa sana kama magonjwa yenye maumivu makali sana, kwenda jela zenye mateso makali kifungo cha maisha, n.k.. kwa kifo chake ni wazi kabisa sasa marehemu kapumzishwa na mateso aliyokuwa akipitia yaliyotuumiza hata sisi, kwanini kwa upande wa pili isizoeleke kufurahia kifo chake endapo kifo kimestopisha hayo maumivu??
Kifo kisikie kwa mwenzio Ndugu yangu
 
Unakuta watoto wanakula butter & chicken huko town, hawamjali mzazi wao siku mzazi akifa kwa homa ambayo ingetibika kwa dozi ya 3,500/= mitoto inaenda kupiga kelele msibani
Hii inakera sana mkuu, mwaka 2019 babu yangu alifariki kwa sababu ya stroke ambayo alikaa nayo zaidi ya miezi 6 lakini alikuwa na watoto wake wa nje hawakuwahi hata kupiga simu tu kuulizia maendeleo yake.
basi siku ya msiba wakaja wanalia tena kwa sauti, baba mdogo ambae alikuwa kiongozi pale aliwapa makavu kuwa waache kulia mara moja, haiwezekani hata kupiga simu tu walishindwa then wapate uchungu akiwa amefariki. Inakera sana.
 
Ikiwa mtu bado anaishi bado kuna tumaini bila kujali yupo kwenye situation gani matatizo huwa yanapita tu
Lakini mtu akifa hakuna tena tumaini kuhusu mambo ya duniani
Kifo kinafikirisha sana

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Na hii ndiyo sababu watu hulia wakiamini chochote kinaweza tokea muda wowote na sehemu yoyote.
Kongole mkuu.
 
Kiulweli kifo cha mtu wa karibu huwa kinauma sana kwa wafiwa kitu kinachotupelekea hata wanaume wazima kujifungia vyumbani kulia machozi hadi kamasi kwa maumivu jinsi yalivyo.

tukiachana na upande wa maumivu, kuna muda unakuta marehemu katika maisha yake alikuwa na matatizo yaliyomtesa sana kama magonjwa yenye maumivu makali sana, kwenda jela zenye mateso makali kifungo cha maisha, n.k.. kwa kifo chake ni wazi kabisa sasa marehemu kapumzishwa na mateso aliyokuwa akipitia yaliyotuumiza hata sisi, kwanini kwa upande wa pili isizoeleke kufurahia kifo chake endapo kifo kimestopisha hayo maumivu??
thinkstupid.png
 
Back
Top Bottom