Pale Nilipoamua kuwanyoosha watu wa kukopesha mtandaoni

Pale Nilipoamua kuwanyoosha watu wa kukopesha mtandaoni

Bani Israel

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Posts
1,775
Reaction score
3,593
Binafsi sio tapeli ila nikiri kwamba niliamua kuwanyoosha hawa wakopeshaji wa mtandaoni baada ya mmoja wao kunichafua,

Nilikuwa mkopaji mzuri wa app fulani jina nalihifadhi nikilipa walikuwa wananiomba nikope tena na tena basi kwangu ikawa kama mazoea kopa lipa

Tabu na mateso vilianza pale niliposhindwa rejesha pesa yao kwa wakati tena hata wiki haikufika lakini chamoto nilikiona, nilipokea meseji za watu nnaowaheshimu ikiwemo wazazi kuwa natangazwa mimi tapeli na nimewaweka wao kama wadhamini, nikaja kujua ni wale watu wa app wanatumia namba za watu wangu wakati sikuwapa hizo namba,

Kweli nilichukizwa kwa kifupi nilikwazika na kughafilika sana na nikaamua sasa kama mbwai iwe mbwai liwalo na liwe siwalipi na nikaamua sasa nilkope app zote niwaonyeshe kazi kuna app walizonipa kuna app walinitosa mana nilichukua hata kama ni buku 7 twende 😁😁.

Usiulize nilikuwa napigiwa simu ngapi kwa siku.
 
FB_IMG_1713347098276.jpg
 
Back
Top Bottom