Pale unaona abiria mwenzako kwenye daladala wanakimbilia kutoka mlangoni na madirishani

Pale unaona abiria mwenzako kwenye daladala wanakimbilia kutoka mlangoni na madirishani

Dah barabarani kuna mambo mengi sana ukifika salama home sema asante mungu
 
Pole sana Mkuu.

Ila wanasemaga hiyo ya kuruka ruka saa ingine hata sio nzuri sababu unaweza kukuta mtu ndo anapata madhara zaidi.
 
Kuna barabara za kuchepuka pale kushoto na kulia sijui kwa nini madereva huwa hawazitumii kidogo zile salama.
 
Nimshukuru Mungu kwa kulinda leo 🙏🏾🙏🏾🙏🏾

Leo hii saa 4 usiku nipo siti ya mwisho kabisa kwenye daladala ya kutokaea Kongowe kwenda Mbagala Rangi 3 kwenye kilima kile baada ya mto kufika Rangi 3 Ghafla naona abiria wenzangu wanakimbilia mlangoni, wengine wanatokea madirishani wengine wanaruka mlangoni.

Nami nikatoka nduki kwenda mlangoni ila sikufanikiwa kutoka maana dereva wa daladala alikuwa anarudi reverse.

Ndio nachungulia mbele naona Malori mawili yanatumbukia moja mtalo wa kulia lingine kushoto na bajaji moja mbele yetu mtalo wa kulia.

Kumbe Lori moja limefeli breki likawa inarudi nyuma. Dereva wa Lori la pili akarudi nyuma kukwepa ndio kuingia mtaloni.

Kama wale madereva waliingizwa malori yao mtaloni makusudi ili wasitusombe magari ya nyumba Mungu awabariki maana sijui ingekuwaje leo.

Yule dereva Bajaji pole yake nadhani hamna aliyeumia kwenye Bajaji.

Asante Mungu, naomba nifike salama leo nyumbani bado naungaunga daladala hadi Pugu usiku huu 🙏🏾🙏🏾🙏🏾
"Mtalo". "Mtaloni". Dah.
 
ila wabongo bwana! Sasa apa mungu anaingiaje?
Mchezo umemalizika, Kocha Mgunda tupe maoni yako ya mchezo wa leo
"Kwanza tunamshukuru mwenyenzi mungu hamdulilah, mchezo una matokeo matatu blah blah..."
 
Back
Top Bottom