Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Waziri wa mambo ya nje wa Palestina Riyad al-Maliki amekataa kuchukua uenyekiti wa jumuiya ya nchi za kiarabu unaozunguka ikiwa ni kupinga kitendo cha baadhi ya nchi za kiarabu kurudisha uhusiano na Israel taifa linalokalia ardhi zao na kuwanyima haki za kuishi.
Amesema kuna heshima gani kwa sisi kuongoza jumuiya ambayo tutakapokuwa mwenyekiti na wao wanaongeza kasi kurudisha uhusiano na adui yetu.
Hatua hiyo ya palestina imekuja sambamba na msimamo wa rafiki mwengine wa karibu wa Palestina,nchi ya Qatar kutoa msimamo wake wa kulaumu jumuiya ya kimataifa ya kutokuikemea Israel iliyoshindwa kutekeleza maazimio yote ya Umoja wa Mataifa kuhusiana na Palestina na wakati huo huo ikiendelea na uvunjaji zaidi wa haki za wapalestina na huku wakiendelea kuwavunjia majumba yao na kuteka ardhi finyu iliyobaki mikononi mwa wapalestina.Kauli hiyo imetolewa hapo juzi na kiongozi wa Qattar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani kwenye kikao cha 75 cha baraza kuu la UN.