Pamba Jiji naiona kama vile ilikuwa ligi kuu misimu minne, wakikaza watasumbua sana

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
4,701
Reaction score
11,920
Wakuu habari,

Jana nimeangalia mtanange kati ya Pamba jiji na Prison Fc.

Nilichokiona
Beki wanajiamini sana kuliko hata Job au Mwamnyeto, wakiwa na mpira hawapigi hovyo hovyo na wwnajua kukaba

Golikipa Amos Yona yupo njema anaokoa mpaka mashambulizi ya counter attack

Winga zipo safi na washambuliaji wapo vizuri

Tatizo
Namba nane na kumi hawajui kupiga pasi za mwisho

Kilichonishangaza
Wanapiga soka safi hawapigi hovyo hovyo

Kumbe yule kocha aliyekuwa Tabora Fc ni kocha mzuri

Wqnapiga soka la chini kwenye uwanja wa nyasi za kulima na mpira unatembea vizuri

Wakuu hii timu kumbe haikwenda yanga mafunzoni kuangalia mafuriko

Ni suala la muda tu

Nawasilisha
 
Hamna Team pale nakwambia...Team haina muunganiko wale wamecheza vile uwanja wa Nyumbani.
Watapigwa sana wasipojirekebisha game za Away
 
Wakuu habari,

Jana nimeangalia mtanange kati ya Pamba jiji na Prison Fc.

Nilichokiona
Beki wanajiamini sana kuliko hata Job au Mwamnyeto, wakiwa na mpira hawapigi hovyo hovyo na wwnajua kukaba

Golikipa Amos Yona yupo njema anaokoa mpaka mashambulizi ya counter attack

Winga zipo safi na washambuliaji wapo vizuri

Tatizo
Namba nane na kumi hawajui kupiga pasi za mwisho

Kilichonishangaza
Wanapiga soka safi hawapigi hovyo hovyo

Kumbe yule kocha aliyekuwa Tabora Fc ni kocha mzuri

Wqnapiga soka la chini kwenye uwanja wa nyasi za kulima na mpira unatembea vizuri

Wakuu hii timu kumbe haikwenda yanga mafunzoni kuangalia mafuriko

Ni suala la muda tu

Nawasilisha
Wamekutana na prison yenyewe mbovu
 
Kweli tunatofautiana upeo wakujua hiki kibaya na kile kizuri,yaani moto waliopelekewa jana na Prisons bado una ujasiri wakuisifia Pamba? Hao nadhani wapiganie kubaki ligi kuu na next match wapo Dodoma.
 
Ngoja tusubiri mechi 15 mkuu
 
Aiseeee Kiongozi, jana niliona kile ulichokisema kuhusu Pamba Jiji. Kama hawatakuja kujichanganya huko mbeleni basi watasumbua sana musimu huu.
 
Back
Top Bottom