Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,978
- 6,739
Basi la wachezaji wa Pamba Jiji FC limepata ajali katika eneo la Bahi mkoani Dodoma majira ya saa 11 alfajiri wakati kikosi hicho kikiwa safarini kutoka Bukoba kuelekea mkoani Morogoro kwa ajili ya mchezo wa Kombe la CRDB Federation dhidi ya Kiluvya United Machi 11, 2025.
Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo imesema chanzo cha ajali hiyo ni kugongwa na lori hivyo kupelekea mshtuko kwa baadhi ya wachezaji.
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetuma salamu za pole kwa timu hiyo kufuatia ajali hiyo.