Hebu jadili kauli ya wakati wanamkata....
"....tumekupata Mh. Mbowe. Na nakuambia safari hii hutoki, huchomoki..."
Na mwaka jana wakati wa uchaguzi akiwa ktk kampeni ktk jimbo lake, aliyekuwa OCD wa wilaya Hai wakati huo alisema;
"....safari hii hushindi ubunge wewe nakuhakikishia..! Umshinde nani wewe Mbowe...!!!? Safari hii hushindi nakuambia...!!"
Duuh , ila hawa UWT wapuuzi kweli kwa sababu strategies zao kum - incriminate ndugu Mbowe ni za kishamba sana...!
Kosa limeanzia na timing na namna walivyomkamata kuonesha kuwa ni mufilisi ktk mipango yao...
Kwa sababu hebu tu - assume kuwa, labda ni kweli Mbowe ni gaidi. Hata hivyo ni nani atawaamini ktk hatua hii kwa sababu UWT - CCM wameshindwa kabisa ku - maintain consistency ktk uongo wao kuhusu sababu ya kumshtaki huyu Mwamba...!!
Yaani RPC au IGP anafanya PC na kuuanbia umma kuwa ana makosa 1, 2, 3 nk lakini mahakamani wanaenda na makosa mengine kabisa...!
Yaani Jeshi la polisi ni moja, lakini kila polisi anatoa sababu zake tu za kumshtaki huyu Mwamba. Lack of consistency...
By the way, iliwezekanaje kwenda kumkamata saa 8 za usiku akiwa hotelini Mwanza mtu ambaye mchana kutwa alikuwa mitaani akifanya vikao vya chama chake kujiaanda na kongamano la katiba mpya ya wananchi kesho yake halafu usrme sababu siyo hiyo..?