LGE2024 Pambalu: Vijana wamesoma mpaka vyuo vikuu lakini ajira zao ni bodaboda na betting

LGE2024 Pambalu: Vijana wamesoma mpaka vyuo vikuu lakini ajira zao ni bodaboda na betting

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Kazi ya serikali ni kuweka maZingira wezeshi kwa watu wake mfano serikali iapaswa kuwa na sera ya viwanda ,kilimo sekta hiZi MBILI zikitiliwa makazot zinauwezo wa kusajiri idadi kubwa ya watu kwa wakati mmoja lnk serikali yetu inaanaZisha sera lkn hajawezamkuleta tija yoyote mfano kilikuwa sera ya kilimo kwanza wakati wa jkiliishia wapi,pia kilikuwa na sera viwanda nayoimeishiwa wapi kwahiyo utaona kuwa Kuna uhusiano mkubwa kati kati yamserikali na ukosefu wa ajira kwa vijana
 
. ...kubahatisha 'betting'
Kama ni kweli basi Loan Board inatakiwa kuunganisha na mifumo ya betting ili akibeti 1000 ikatwe mia ya loanboard hivyo betting iwe 1100. Na alipata akatwe asilimia 15 ya mikopo wake uliobaki!!!
====
Hii ni kama tumekubali kuwa hii ni ajira Rasmi!!!
Naandika haya lakini nimekasirika!!!
 
Mkuu tusijipooze kwa visingizio vya jumla. Ni graduate wangapi wana hayo majukumu mazito? Graduate walioanzisha familia baada ya chuo sidhani hata kama wanafika 10% na kama mtu alianza familia akiwa hana uhakika wa uchumi wake nao ni upumbavu mwingine (tusiuongelee)

Amini nakuambia graduate asiyeweza kutunza wastani wa Tsh. 1500/- kwa siku ni kaamua yeye mwenyewe na upumbavu wake. Tusikae kutetea ujinga lazima vijana tupeane hasira ya mafanikio.

Kuna jamaa hapa jukwaani wiki iliyopita aliweka uzi amefanya ziara kutoka kanda ya ziwa ameenda kuangalia fursa maeneo ya Morogoro alieleza mengi sana kwenye huo uzi na namna nmaeneo yalivyo na uwezo wa kuzalisha mali.

Na akaeleza anashangaa kuona vijana hawapo active hayo maeneo.

Graduate anatakiwa kupambana yeye binafsi sawa na walivyopambana mababu tukaupata uhuru 1961 wale wazee walikubali kupoteza sehemu ya maisha yao sababu yetu sisi na sisi leo tumekuwa wavivu na waoga wa kufanya mambo.

Hii ni aibu kubwa.
Unafikiri amboa hawana hela au maskin hawapambani unajidanganya sana
 
Unataka mazingira gani zaidi ya hii amani iliyopo na huu uhuru wakuzurura sehemu yoyote ndani ya Taifa hili?. Yapo maeneo ardhi ekari 1 unauziwa na halmashauri ya kijiji kwa Tshs. 50,000/- hadi hata chini ya hapo na hayo maeneo yapo tu wazi mapori.

Vijana wakiambiwa wanaanza kuleta visingizio mara uchawi mara ni mbali na ujinga mwingi. Wanaenda kununua vigogo maelfu ya hekari huko na vijana wapo wapo tu.
Betting
Muziki
Visungura/double kiki
Fegi
Pool table
Mpir
Madem
 
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA taifa John Pambalu akiwa mkoani mwanza wakati wa kufanya kampeni kuwanadi wagombea wa chama chake kuelekea uchaguzi serikali za mitaa amesema vijana wamesoma mpaka vyuo vikuu lakini hawana ajira, ajira za zo ni mbili akiwataja bodaboda na wanaofanya michezo ya kubahatisha 'betting'

Soma pia: Vijana wahitimu wa Vyuo Vikuu wanataka nani awapambanie?
View attachment 3159362

Chanzo: Arusha zone news
Sasa kama watu hawataki kuwapa vijana NSSF yao mapema wajitafutie miradi ya kufanya kwanini wasibet ?
 
Back
Top Bottom