Pambano la Bongani na Majiha lina utata,suluhisho ni hili

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Baada ya pambano la jana kati ya Fadhili Majiha na Bongani Mahlangu kumalizika kwa utata baada ya pambano kuchezwa kwa raundi 10 tofauti na raundi 12 kama mabondia walivyosaini.

Kikawaida mapambano ya mikanda ya WBC huchezwa kwa raundi 10 isipokuwa kwa mikanda ya WBC Silver na WBC gold belt ambayo huchezwa mpaka raundi 12.

Mimi ninavyooona huo mkanda ubaki wazi (Vacant) na itangazwe mandatory fight haraka iwezekanavyo ili pambano lirudiwe tena .

Kinyume na hapo hawakumtendea haki hata kidogo Proffesor Mahlangu Bongani kwa kuwa ngumi ni mchezo wa mahesabu na hatujui Proffesor alipanga nini kwenye raundi zilizobaki maana Proffesor ni mtu wa kubadilika badilika kila raundi ,mara acheze kama orthodox mara southpaw nk.
 
Nakuunga mkono.

Watz tuna usaniii usanii mwingi kwenye kila jambo tunalolifanya. Hili ni kati ya matatizo yanayotuponza tunapotoka nje, kwasababu tunakuta kule hakuna mbeleko tulizozizoea. Tumeshakariri kuwa katika ardhi ya nyumbani ushindi ni wa lazima, matokeo yake tunautafuta kwa kila namna, hata kama haina haja ya figisu sie tunaziweka tu. Mfano katika hilo pambano, yule bondia mtz alikuwa kashalimudu sana na alikuwa anaonekana kuelekea kushinda hata kwa raundi 12, ila kwakuwa figisu hiyo iliingia tayari imeuharamisha ushindi wake.

Mwishoni pale kwenye mahojiano nilimsikia yule sijui ni promota, akisema eti huyo msela wa sauzi hana cha kulalamikia kwakuwa kazidiwa kwenye pambano zima. Hoja za namna hii ni za kijinga na kingumbaru tunazoweza kuzisikia huko uswekeni kwenye vilinge vya gongo na kahawa, zinaonesha ni namna gani mzungumzaji ana uwezo kiduchu upstairs na anaowaeleza anawaona akili ndogo zaidi, na ajabu ni kuwa watu wanamsapoti na kumshangilia!

Kwa akili ya kawaida tu haihitaji aje mzungu au mganga wa kienyeji apige ramli ili kujua kuwa kwenye masumbwi konde moja tu linatosha kubadili matokeo ya mchezo, achilia mbali raundi mbili.

Nilimwelewa sana msauzi alipolalamika, kwani huenda alikuwa na mipango yake kule mwishoni mwa pambano, na pambano limeanza tukijua ni raundi 12 kama alivyosainishwa.

Pambano lirudiwe na lieleweke mapema ni la raundi ngapi. Jamaa mtz yule ana uwezo wa kutosha kumshinda tena yule babu, lakini ashinde kihalali, asichafuliwe CV yake kwa kuonekana anashinda kiutata utata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waangalie mfano mzuri kwa Tony Rashid kilichomtokea kwenye pambano lake la kwanza dhidi ya Mahlangu Bongani.
 
Back
Top Bottom