Pambano la Mfaume Mfaume na Iddy Pialali lavunjwa raundi ya kwanza

Pambano la Mfaume Mfaume na Iddy Pialali lavunjwa raundi ya kwanza

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Licha ya kusubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi wa mchezo wa ndondi, pambano hilo limeishia Raundi ya Kwanza kutokana na Iddy Pialali kupata majeraha baada ya kugongana na mpinzani wake.

Wakati wakirushiana makonde Pialali alionekana akilalamika, baada ya mwamuzi kusimamisha ndipo ikabainika kuwa alichanika karibu na jicho, pia kutokana na damu kuvuja kwa wingi alishindwa kuendelea na mchezo huo.

Fk7r3WdXoAIhre2.jpg
Fk7r181XEAA4FU3.jpg
 
Hawa walitaka wamalize TU pambano maana hata kuingia ilichukua mda sana wanabahati Arusha wanyonge dar wangerudisha hela
Wa kwanza kutakiwa kuingia uwanjani ni Mfaume, dogo kaitwa mara tatu imemchukua dakika zaidi ya 11 ndipo anaingia uwanjani,

Yule Pialali kaingia muda on time, hivyobasi inaniwiwa kusema Mfaume kuna viashiria vya mambo ya kiswahili.

Halafu kubwa zaidi hana Fair Play, jamaa (Pialali) mstaarabu na anajua nini ngumi, all in all Promota aandae pambano warudiane.
 
Yani utadhania kuna la maana kwenye ndondi Tanzania!
 
Mapambano ya Jana mengi Sana yalikuwa ya hovyo kabisa, Kama sikosei mawili ndio yalikuwa mapambano ile yalobaki ni walevi tu.
Pambano la Mfaume Mfaume na Pialali, Kama lilipoishia ingekuwa wanahesabu point Mfaume alipigika.
Na nadhani Mfaume aligundua Kuna kudharirika pale, akatumia mbinu za medani
 
Wa kwanza kutakiwa kuingia uwanjani ni Mfaume, dogo kaitwa mara tatu imemchukua dakika zaidi ya 11 ndipo anaingia uwanjani,

Yule Pialali kaingia muda on time, hivyobasi inaniwiwa kusema Mfaume kuna viashiria vya mambo ya kiswahili.

Halafu kubwa zaidi hana Fair Play, jamaa (Pialali) mstaarabu na anajua nini ngumi, all in all Promota aandae pambano warudiane.
Mfaume alikuwa anapoteza hili pambano maana hata fitness na confidence ya Pialali ilikuwa juu sana
 
Mfaume muhuni ameleta boxing ya kiswahili Sana.. aliogopa kupigwa mbele ya mama yake mzazi .....Nimemdharu

Mwakinyo remain professional boxer in Tanzania.
 
Back
Top Bottom