Pamela Maasay ashinda Ukatibu Mkuu BAWACHA, amwaga Catherine Ruge

Pamela Maasay ashinda Ukatibu Mkuu BAWACHA, amwaga Catherine Ruge

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Snapinst.app_470176979_18452306782071244_1748752624688052621_n_1080.jpg

Pamela Maasay
Pamela Maasay amechaguliwa kuwa Katibu wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) akimbwaga Catherine Ruge aliyeshindwa kutetea nafasi hiyo.

Pamela ameibuka kidedea kwa kura 37 sawa na asilimia 54 katika kinyanganyiro hicho huku Catherine akipata kura 34 sawa na asilimia 40 na mgombea mwingine Esther Daffi akipata kura 15.

Uchaguzi uliompa ushindi Pamela kuiongoza Bawacha umefanyika leo Januari 18, 2025 Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Mbali na nafasi hiyo, Nuru Ndosi ametetea nafasi yake ya Naibu Katibu Taifa-Bara kwa kura kupata 42 akimbwaga mpinzani wake wa karibu Glory Latamani aliyepata kura 31 na Neema Mhanuzi akipata kura 11.

CHANZO: MWANANCHI
 
Ruge wa hovyo sana, aliingizwa chaka akajiunga na chechemela
 
Back
Top Bottom