Pamoja na aibu tunayoipata kimataifa lakini pia tunapoteza pesa nyingi ambazo zingefanya mambo mengi

Pamoja na aibu tunayoipata kimataifa lakini pia tunapoteza pesa nyingi ambazo zingefanya mambo mengi

Deadbody

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2015
Posts
4,274
Reaction score
6,595
Rais naomba wafikirie vizuri hawa Stars,hizi pesa zingepelekwa kwa wanafunzi wa elimu ya juu wapate mkopo.
 
Ni upuuzi kila siku sisi wa kufungwa tu bora tuangalie dili zingine....
 
pccb wasimamie soka letu wajue kule kuna ajira na kodi ya serikali, wawasimamie hawa simba na yanga waache kununua mechi, ndio tutapata wachezaji wa ukweli , hawa kina kichuya wanaopata hat-trick kwenye timu zilizonunuliwa wayajiishia,
 
Tuchague wachezaji wenye maumbo makubwa.. Timu nzima wawe futi sita hatufungwi tena
 
kwani hizo pesa ni za serikali? na kesho utaleta thread ya pesa wanazotumia wasanii wa bongo kwenda kushuti south zikachonge madawati kwa sababu wanakosa tuzo.
 
Sasa kila timu inayofungwa ikiwa itajitoa mchezoni, baadaye mchezo wenyewe si utakufa?
Tanzania kufungwa na Zimbabwe si ajabu. Ni kama Argentina kufungwa na Brazil.
 
pccb wasimamie soka letu wajue kule kuna ajira na kodi ya serikali, wawasimamie hawa simba na yanga waache kununua mechi, ndio tutapata wachezaji wa ukweli , hawa kina kichuya wanaopata hat-trick kwenye timu zilizonunuliwa wayajiishia,
Misingi ya soka tunaifuata? nayo ni uwekezaji toka chini zamani kulikuwa na sera michezo mashuleni kama umishumta na umisseta hii ilisaidia kuona vipaji vya vijana. Ukija makazini kulikuwa na shimuta na shimiwi hii iliwafanya wafanyakazi kuwa na afya njema na pia taasisi zote zilikuwa na timu kama sigara, plisner, ndovu ,RTC TANESCO kwa kuwa miaka hiyo shule hazikuwa nyingi so vijana wengi hawakuchaguliwa kuingia kidato cha kwanza hivyo basi waliokuwa wanamichezo hodari walijiunga na timu hizi kama vibarua lakini kazi yao ilikuwa michezo hasa mpira wa miguu na mpira wa pete kama ni wilayani kijana anacheza pale daraja la nne akifanya vizuri mwaka unaofuatia timu nyingine zinamchukua na kuendelea nakumbuka miaka hiyo wakulima wa pamba walikatwa pesa nadhani ilikuwa shilingi 5 kwa kila kilo pia majimaji enzi za mzee gama penye mafuta walikuwa wanakatwa kuchangia timu hayo mambo huwezi kuyafanya sasa hivi kwa style hiyo.
Sasa serikali iliwekeza penye michezo kwa mtindo huo na ilipojitoa anguko lake ndio hili tunalo liona kuna mdau kazungumza kuhusu maumbo hili nalo ni changamoto nadhani alikuwa ni claudio reloy kocha wa Cameron kuna siku katoka younde na kuvinjari nje ya jiji akakuta watu wameutenga wanapiga ndiki kavutiwa kuangalia akamuona mtu mmoja shababi hivi anafanya mambo yake kavutiwa baada ya mchezo kamuita na kumhoji jamaa akajibu huwa tukitoka kupalilia mikokoa yetu basi huja hapa kuchangamsha miili akampa namba na nauli kuja mjini jamaa huyo alienda world cup na goli alifunga raymond kalla ila kwa kuwa umri ulikuwa umekwenda hakuwika sana.
Mambo yanabadilika wazazi siku hizi utadhani wanazaa wabongo flavour sio kweli ila ule muamko wa soka umepungua open spaces zote mmeuza huo ushawishi utatoka wapi? Tupate kina said salim bakhresa kama kumi hivi mpira utarudi na sio figisu figisu hizi tutegemee maajabu na malalamiko mengi Messi kaenda la masia ana miaka 13 mpaka leo anacheza mpira tu sisi kwa sababu huyu mtu alizifunga yanga na simba basi tunamchukua wakati ile misingi ya mpira hana kujiweka katika nafasi jinsi ya kupokea mpira hajui jamani aaah
 
Back
Top Bottom