Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 37,630
- 47,434
Hawa Ewura naona wanamkakati wananchi tutembee kwa miguu katika shughuli zetu za kila siku.
Pamoja na gharama za maisha kuwa juu bado bei ya mafuta imepanda kwa Tshs. 149 kwa lita.
Mafuta ni bidhaa muhimu sana katika uchumi wa nchi hivyo kama yakipanda bei basi ni mara moja tu madhara yake huonekana katika mambo mengi ikiwemo gharama za usafiri bei za bidhaa na vyakula nakadhalika.
Hapo nyuma tuliwahi elezwa kwamba serikali inatia ruzuku ya bilioni mia ili kunusuru bei ya mafuta.
Pamoja na jitihada hiyo bado bei inazidi kupanda na gharama za maisha nazo zitaendelea kuwa juu.
Serikali ituambie inampango gani katika jambo hili kwani historia inatufundisha kwamba kwa hapa Tanzania bei ikishapanda kushuka ni majaliwa tena.