KERO Pamoja na hali ya usafi wa vyoo vya umma inaeleweka. Vyoo vile kwa walemavu wanaotambaa ni jehannam

KERO Pamoja na hali ya usafi wa vyoo vya umma inaeleweka. Vyoo vile kwa walemavu wanaotambaa ni jehannam

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Kalaga Baho Nongwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2020
Posts
9,953
Reaction score
23,150
Wakuu inaumiza, inakoroga na kukata maini kabisa. Fikiria kwanza vyoo vya umma vinavyoshughulikiwa kila baada ya dakika 6. Masizi, michanga, matope na chembechembe za vinyesi zinayotapaa pale ambapo zoezi la kuflash likitumi nguvu zaidi.

Anakuja mlemavu anatembelea mikono na miguu anaingia. Anajisaidia anatoka, yani wewe tu na uzima wako unatembea na miguu iliyovaa viatu muda mwingine unasita kabisa kutumia choo kile. Mlemavu ndo anasaga magoti,mikono na makalio yanaburuta pale.

Soma Pia: Kwanini vyoo vya umma vinatengwa kwa jinsia ya wanaume(ME) na wanawake(KE)?

Leo nimepishana na mlemavu choo cha umma kariakoo nusu nilie. Yani hali ile wakuu sio njema kabisa. Ina mana teknolojia imeshindwa kuwatafutia suluhu hawa watu kwenye vyoo vya umma?

Kalaga baho
 
Tatizo ni madiwani na watendaji wa halmashauri, hili jambo si la kufikiri mara mbili ni kuamua tu. Hata wangetengewa chumba kimoja wanaume na wanawake kingetosha kwa kuwa siyo wengi kiivyo!
 
Tatizo ni madiwani na watendaji wa halmashauri, hili jambo si la kufikiri mara mbili ni kuamua tu. Hata wangetengewa chumba kimoja wanaume na wanawake kingetosha kwa kuwa siyo wengi kiivyo!
Walemavu wawe na vyoo vyao? Vimilikiwe na manispaa? Kwa nn wasipate aiding tools za kuwa salama zaidi mana zoezi la kuwa na vyoo vyao linaweza kuwa gumu kwelikweli. Maeneo mengi ya mjini vyoo hivi ni mali za watu binafsi ukiachilia mbali vile vya sokoni
 
Maeneo mengi ya umma kuna vyoo kwa ajili ya walemavu na vinawekewa alama hii ♿. Siyo vyoo tu hata kwenye huduma nyingine ya kijamii kuna sehemu ya walemavu na huwekewa alama hii ♿.

Watu binafsi wanaojenga vyoo vya biashara ni kupewa maelekezo tu wala haina tatizo.
 
Maeneo mengi ya umma yanajumuisha maeneo gani mkuu?
 
Mwaka 2019 nilikuwa maktaba ya Taifa nasoma , nilipoenda Katika vile vyoo Aisee vilikuwa safi Sana na walikuwa wameweka vyoo vya watu wote ikiwemo vya walemavu .

Nadhani maktaba ya Taifa inaweza kutumika watu kwenda kujifunza kitu pale.

Wanapojenga public toilet kitaalamu lazima waweke na vyoo vya walemavu

Ila hawa jamaa wanajijengea tu ilimradi.
 
Mwaka 2020 nilitembelea stend ya ubungo Ila nilishangaa kuona vile vyoo vilivyo vichafu maji hamna

Sehemu inoyoingiza mabasi zaidi ya 300 kuwa na miundombinu Kama ile.

Ukienda Temeke mwisho stend hauwezi hata kutumia vile vyoo Kwa jinsi vilivyo vichafu.

Tunasafari ndefu ya kwenda.

Sasa hao walemavu si ndo hatari kabisa.
 
Back
Top Bottom