Asprin
JF-Expert Member
- Mar 8, 2008
- 68,223
- 96,083
Mimi sidhani kama kuwa happy kunasababishwa na ndoa au kua single kwa sababu mambo ambayo yanaweza kukusababisha usiwe na furaha yapo hata ukiwa na umeoa/olewa au hujaoa/olewa. Kama hujaolewa ukichukulia bila ndoa sitakua na furaha basi hutokua na furaha. Na kama umeolewa ukichagua mimi mume wangu akirudi amelewa sitokua na furaha na kweli hutokua na furaha ila ukiamua ulevi wake hauwezi ninyima furaha basi utaishi kwa amani zote, tena siku nyingine utakua unamuuliza baby leo hunywi. Kwa nini watu wanaonywa kuwa usishike simu ya mwenzio si kuogopa kujipa maumivu? unapenda kushika lakini ukifikiria maumivu yake mwenyewe unatuliza kitenesi. Na upweke hivyo hivyo ukiuwazia sana ni sawa sawa nakupekua simu ya mwenza wako. Ishu ni kuamua tu kuwa na raha au usiwe nazo. Ti aliniambia siku moja pale feawei kwamba dada yangu usicomplicate maisha yafanye tu yawe marahisi nawe utaishi kwa amani
Aisee leo Maty umeamua kuwa mama wa busara.
Hii sredi umeitendea haki sana.
Thanks
Swali la kizushi: We unalala na mto au na limjamaa lenye miguu mitatu?