Pamoja na machache yanayoyesemwa, TRC imefanya kazi kubwa - Kihenzile

Tanzania Railways Corp

Govt Institution
Joined
Mar 23, 2018
Posts
292
Reaction score
690
Naibu Waziri wa uchukuz, Mhe. David Kihenzile, amesema Reli ya Kisasa (SGR) inaendelea kuwa kichocheo muhimu cha biashara, uchukuzi, miundombinu na ukuaji wa uchumi kwa kuwezesha usafirishaji wa abiria na mizigo kwa haraka, usalama na ufanisi.

Mhe. Kihenzile, ameyasema hayo Julai 06, 2026 alipotembelea banda la Shirika la Reli Tanzania (TRC) katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), yanayoendelea jijini Dar es Salaam, ambapo Mhe.Kihenzile, alisema maendeleo ya reli yanafungua fursa zaidi za biashara na uwekezaji, huku akiwahimiza wananchi na wafanyabiashara kuitumia huduma hiyo kuongeza tija katika shughuli zao za kiuchumi.

Katika hatua nyingine, Mhe. Kihenzile, aliipongeza TRC kwa kuendelea kuboresha huduma na kutoa elimu kwa wananchi kupitia maonesho hayo, akieleza kuwa hatua hiyo inaongeza uelewa wa wananchi kuhusiana na Shirika la reli.

Soma Pia: TRC yaingiza Ford Rangers zenye teknolojia ya Laser kukagua Reli ya SGR

“Huduma za reli hususani ya SGR, zimeleta mapinduzi katika usafirishaji wa abiria na mizigo kwa kuokoa muda, usalama na ufanisi, hatua inayorahisisha shughuli za wafanyabiashara na kuvutia uwekezaji wa ndani na nje," alisema Mhe. Kihenzile.

IMG-20260706-WA0023.jpg
IMG-20260706-WA0027.jpg
IMG-20260706-WA0026.jpg
 
View attachment 3623878View attachment 3623879View attachment 3623880
NIMESOMA UPUMBAVU!
 
Back
Top Bottom