Pamoja na matokeo ya jana ila Simba bado atafuzu kwenda robo fainali

XII Tz

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2020
Posts
4,345
Reaction score
7,076
Habari wakuu

Kwanza niwape pole wanasimba wenzangu kwa kilicho tokea jana, itoshe tu kusema kwamba Raja wametuzidi mno, ni maji marefu sana kwetu hivyo kukaa na kuhuzunika haitosaidia wala kubadilisha msimamo wa kundi.

Pili niwape hope wana simba wenzangu kuwa chance ya sisi kutoboa makundi bado ni kubwa mno, tumebakiwa na mechi nne za makundi mkononi ambazo kimahesabu zinatosha sana kutupeleka robo fainali.

Kwanza kabisa tuna mechi mbili dhidi ya vipers yaani home & away pia mechi za marudiano dhidi ya Raja na Horoya. Jana hatukucheza vibaya bali quality kubwa ya Raja ili tuhukumu kama nilivyosema hapo awali, lakini kiwango kile kile tukihamisha dhidi ya vipers na Horoya simuoni yeyote anaye chomoka.

Kwanza mpaka sasa tufahamu kuwa raja ameshajitenga tuliobaki tunagombea nafasi ya pili, ambapo mpinzani wetu mkubwa ni Horoya kutokana na msimamo wa kundi ulivyo, Horoya mpaka sasa ana point nne na mechi nne mkononi ambapo atakutana na raja home and away pia marudiano na vipers na Simba.

Kwa namna yeyote ile Horoya hana quality ya kumfunga Raja labda akijitahidi sana anachukua sare nyumbani ila ni obvious kwamba atampiga vipers ambapo pia sio rahisi kutokana na uchezaji wao. Hivyo kama atamfunga vipers kwa alama zao nne ambazo tayari wamezivuna atafikisha alama Saba na endapo atapata angalau sare basi atafikisha alama 8, hawezi kuvuka hapo, ila binafsi namtazamia kwenye alama 7 sababu raja hawana utani.

Turudi sasa kwa mnyama simba, binafsi nitakuwa wa mwisho kuamini kama Horoya ataondoka na point kwa mkapa, hivyo ni obvious tutampiga, kama Horoya ameweza kupata sare pale st Mary's kitende dhidi ya vipers basi tunao uwezo wa kumpiga vipers pale pale kwao japo sio rahisi ila inawezekana, na akija kwa mkapa apasuke pia, mpaka hapo tutakuwa na alama 9 ambazo Horoya kwa moto ule wa raja hata aroge hawezi kufikisha.

Alafu mechi iliyobaki ya marudiano dhidi ya Raja Casablanca, tukafe nao huko huko watupige hata kumi, ila tutakuwa tumefuzu kwenda robo fainali Nyuma yao, hivyo wanasimba nafasi bado ipo tusikate tamaa, nguvu kubwa tuielekeze kwa vipers na Horoya..

Nguvu moja [emoji881]
 
Hizi hesabu ni za matumaini ila Kwa sasa la kufikiri ni kushinda mechi zinazofata ili kuiweka sawa heshima ya Simba na sio kuingia robo fainali. Ikitokea katika kushinda kwako wengine wakashindwa ukapita unakuwa umebahatisha.

Ukishaanza mambo ya kumtegemea Raja ambaye hata akidondosha p3 hana la kupoteza akushindie mechi ili upite tayari ni hesabu za bahati nasibu. Unabeti
 
Ulichonifurahisha umedeclare kabisa Kwa Raja hampati hata point moja, mtakwenda kupunguza idadi ya magoli tu.

Ile discipline ya Jana inaitwa Mwana ukome mpaka saa hizi Ahmed Ally hana hamu amelala na kispika chake.
 
Mechi ya jana mimi wala haukuniumiza matokeo yake

Kwenye madraft unapokutana na mchezaji mkubwa kukuzidi wewe kuna kauli moja ya utani tunapenda kuitumia kuwa "draft linamuheshimu fundi"

Hata ukikosea ila hauwezi ukakosea katika level sawa na huyu asiyejua

Kwa hiyo sisi tulifanya makosa lakini haina maana wao Raja hawakufanya makosa, ila namna ya ku convert hayo makosa kuwa magoli ndio hapo mpira ulipoamua kumpa advantage fundi
 
Ulichonifurahisha umedeclare kabisa Kwa Raja hampati hata point moja, mtakwenda kupunguza idadi ya magoli tu.

Ile discipline ya Jana inaitwa Mwana ukome mpaka saa hizi Ahmed Ally hana hamu amelala na kispika chake.
Ahmedy Ally ame play role yake kuhusu hamasa na kweli uwanja ulijaa

Swala la matokeo ni part ambayo inawahusu wachezaji na ndio waliomuangusha

Kuna uwezekano muda ataoamka Ahmedy Ally ndio muda ambao Ally Kamwe atakuwa anaenda kulala

You never know
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mechi ya jana mimi wala haukuniumiza matokeo yake

Kwenye madraft unapokutana na mchezaji mkubwa kukuzidi wewe kuna kauli moja ya utani tunapenda kuitumia kuwa "draft linamuheshimu fundi...
Kabisa mkuu ila Simba anatoboa ..
 
Na ndio mpira ulivyo ila kutoboa tuna toboa.
 
Habari wakuu

Kwanza niwape pole wanasimba wenzangu kwa kilicho tokea jana, itoshe tu kusema kwamba Raja wametuzidi mno, ni maji marefu sana kwetu hivyo kukaa na kuhuzunika haitosaidia wala kubadilisha msimamo wa kundi.
...
Simba hawezi kumfunga Vipers kirahisi hivyo.
 
Wala sikupingi kabisa, sometimes bahati inahusika pia.

Mbona Simba ile iliyokung'utwa HAMSA HAMSA ilifuzu hadi kufikia robo fainali?

INAWEZEKANA KABISA.
Mkuu, Simba anapita mchana kweupe ila ndo hivyo hawa ndugu zetu wameamua kutukatisha tamaa ila hata wao ukweli wanaujua, mbaya zaidi wamesahau kuwa Tp mazembe ana wangoja jioni ..
 
Habari wakuu

Kwanza niwape pole wanasimba wenzangu kwa kilicho tokea jana, itoshe tu kusema kwamba Raja wametuzidi mno, ni maji marefu sana kwetu hivyo kukaa na kuhuzunika haitosaidia wala kubadilisha msimamo wa kundi...
Safari ya matumaini itaanzia tarehe 25. Simba akifungwa Uganda basi shughuli itakuwa imeishia hapo
 
Ahmedy Ally ame play role yake kuhusu hamasa na kweli uwanja ulijaa

Swala la matokeo ni part ambayo inawahusu wachezaji na ndio waliomuangusha...
Tunawaheshimu TP Mazembe lakini Kwa usajili wa Yanga hawa ni size yetu kabisa, tunahitaji point 3 muhimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…