Unapozungumzia kukubalika hakuna mwanamuziki aliewahi kukubalika duniani kote na kupendwa kama Michael Jackson,ukweli kuwa hit songs zake zilikuwa zinaingia top ten katika nchi tofauti kwenye mabara tofauti,ukweli kuwa show zake zilikuwa zinajaza mpaka kutapika katika nchi tofauti na mabara tofauti,ukweli kuwa maisha yake yalikuwa yanaleta mgawanyiko wa kimawazo katika nchi tofauti tofauti na mabara tofauti,ukweli kuwa muziki wake ulikuwa unaimbwa na kueleweka na watoto,wadada,wamama na wababa, ukweli kuwa nyota ya umaarufu ilianza kumfuata akiwa na miaka chini ya kumi,(kimsingi umaarufu ndio ulimpenda, kumtafuta,kumfuata na kuambatana na Michael na wala hakuutafuta kiivyo kwani Michael mwenyewe alikuwa mtu wa aibu sana nje ya jukwaa lamuziki).Ukweli kuwa kifo chake kiliushtua zaidi ulimwengu kiasi kuwa mtandao wa google uliripotiwa kustack kwa muda kwa idadi kubwa mno ya watu walioingia mtandaoni kutafuta habari zake!
kweli zote hizo na nyingine nyingi zinamfanya Michael asiwe na upinzani kwani aliunyanyua muziki na kuupeleka level za juu kabisa kiasi kuwa wasanii wote waliofuata baada yake walikuwa ama wanalinganishwa ama wanataka kulingana nae mfano Chriss Brown.
Bob Marley ana heshima zake pia,kwani aliupa umaarufu kiasi muziki wa reggae ingawa hata hivyo waliouelewa walikuwa wachache sana kwa wakati huo, kimsingi jinsia ya kike hawakuuelewa kihivyo(kumbuka jinsia ya kike ni mojawapo ya vigezo visivyo rasmi vinavyoongeza umaarufu wa wasanii kwa ushabiki wao uliojaa mahaba).Muziki wake ulikuwa mzuri ingawa aliimba kivivu vivu,mi binafsi namkubali zaidi Lucky Dube anachangamsha na ujumbe mzito zaidi kuliko Marley.kwangu Michael alikuwa anakubalika zaidi kuliko Marley,ingawa kimsingi tunapaswa kushukuru kuwa hawa watu wawili walipita katika ulimwengu huu na kutuachia kumbukumbu na alama za kukumbukwa sana.