Pamoja na Tume Huru ya Uchaguzi, isiwe lazima kila jimbo kuwa na mbunge

Pamoja na Tume Huru ya Uchaguzi, isiwe lazima kila jimbo kuwa na mbunge

Patriot

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2008
Posts
5,705
Reaction score
4,703
Leo Bunge limeahirishwa. Michango tumeiona kwa ubora tofauti. Hapa Ndani ya JF kuna watu wanashawishi watu fulani waende majimboni kuchukuwa nafasi za Ubunge.

Niliwaona Ukerewe wakiwaomba maprofesa, nawaona leo wana Karagwe wakimuita Profesa.

Ombi langu ni kwamba isiwe ni lazima kila jimbo liwe na mbunge. Yaonekana kuna wakati watu wa ubora wa chini sana wanachaguliwa kushika nafasi za ubunge kiasi cha kushindwa kuwasaidia wananchi. Ndani ya Bunge, inakuwa ni mchanganyiko wa viwango tofauti!

Inapoonekana jimbo halikupata mtu wa kiwango kinachokubalika, isiwe lazima kuweaka mtu yeyote. Nasema tena isiwe lazima kila jimbo kuwa na mbunge.
 
Patriot,

Kikiwekwa kiwango PhD, Master's, Form six, Kibajaji, Msukuma na wengine wa aina hiyo watakubaliana na hilo?
 
Back
Top Bottom