funaku
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 39,468
- 31,952
Tafakuri yangu ni moja na ya msingi sana.
Kama Taifa hatuna ushahidi usio na mawaa eti matatizo au changamoto tulizonazo zinatokana na katiba kuwa ya zamani.Hakuna ushahidi wa kisayansi ulioweza kunishawishi eti katiba yetu ni mbovu.
Nilichoshuhudia na nilichosikia na nilichokifuatilia katika siasa zetu ni baadhi ya wanasiasa kutafuta kete inayotisha ya kujinadi.
Hakuna mwanasiasa aliyeweza kujadili na kutanabaisha kwa uwazi ni maeneo yapi haswa ya katiba iliyopo yana changamoto na ni nini anashauri kiwekwe.
Kwa muktadha huu ninaona kuna kundi la wapiga kelele,wanunuliwa na wahuni ambao hatujawapigia kelele za kutosha au kuwapa hoja kuntu kuhusu swala hili.
Bado tunayo katiba imara ambayo haijatejekelezwa kikamilifu.
Kwa maoni yangu kuna kundi la wahuni na waliolipwa kutaka agenda hii iende mbele kwa manufaa binafsi na sio manufaa ya umma.
Kenya na Afrika Kusini zimekuwa na katiba mpya lakini hakuna la maana kwa wananchi wanyonge....hili ni somo muhimu.
kwa kuwa mchakato wa katiba mpya ulifanyika na ukaishia katikati this time ukifanyika usitumie gharama yoyote...wanaoitaka katiba mpya wasilipwe chochote.
Kwa ufupi :Tanzania inahitaji maendeleo na matokeo katika kazi ...huu sio muda wa blah blah na majadiliano yasiyokwisha.
Katiba mpya sio kipaumbele cha mwananchi aliopo Mpitimbi au bukundi au kwa msisi au ukerewe.
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!