Pamoja tunaweza kuwapatia tabasamu | furaha ya mtoto ipo kwenye mambo madogo sana ya kidunia

nergomafioso

Senior Member
Joined
Apr 3, 2024
Posts
158
Reaction score
362
Habari za wakati huu waungwana, natumaini Mungu anaendelea kutujaalia uzima mpaka siku hii ya leo.

Natumaini humu jukwaani tupo watu wa imani mbalimbali, kwa ndugu zangu wakristo leo ni ijumaa kuu siku ambayo wanaomboleza kuteswa na kufa kwa Yesu Kristo.

Hivyo basi siku ya jumapili 20/04 wakristo wote watasheherekea Pasaka sikukuu ya ufufuo wa Yesu Kristo .
Najua wengi wetu tumetokea katika familia tofauti kiuchumi ila kuna upande wa pili ndugu zetu wanaishi maisha ambayo kwa kuhadithiwa tu bila kuona kwa macho huwezi kuamini kama kuna binadamu anaishi maisha haya.

Kifahamu kijiji cha Lumbiji kilichopo wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
• Kijiji cha Lumbiji kipo umbali wa kilometer 78 kutoka wilaya ya Kilosa na kilometer 162 kutoka mkoa wa Morogoro na kilometer 358 kutoka Dar-es-salaam.
• Wenyeji wa hichi kijiji ni wakaguru pia kuna muingiliano wa makabila mengine kama wamasai na wasambaa wanaohamia kwa shughuli za kilimo na ufugaji.
• Kijiji hiki kinapatikana juu ya milima mikubwa na misitu minene ya kitropiki kutokana na miundombinu kuwa hafifu kunafikika kwa kutumia pikipiki na baadhi ya wenyeji hutumia baiskeli ingawa ni hatari lakini ni sehemu ya maisha yao.
• Huduma za kijamii ni changamoto kwa wakazi wa kijiji hiki÷
° Watoto wanatembea umbali mrefu kwenda kupata elimu.
° Miundombinu ni mibovu mnoo hali inayopelekea ugumu katika shughuli za kibinadamu waishio kijijini hapa.
° Huku umeme wa Tanesco hawaujui kabisa, wanakijiji wanatumia solar power na generators (engines) kama chazo kikuu cha nishati. ila nimeona kuna nguzo za umeme zimepita msituni kuashiria karibuni wakazi wa Lumbiji watapata umeme.
° Huduma za kiafya ni tatizo kubwa linalosumbua wakazi wa kijiji hiki, huduma zinatolewa na kanisa la Roman katika kituo kidogo cha afya kisicho na wabobezi wa magonjwa makubwa kupelekea wagonjwa kulazimika kwenye hospital ya wilaya ambapo wataweza kupata huduma bora na wengine hushindwa kufika uko kutokana na kushindwa kumudu gharama za usafiri na matibabu na kupoteza maisha kwa kukosa huduma msingi za kijamii.
° Wakazi wengi wa lumbiji wanategemea kilimo kuendesha maisha yao ya kila siku na wamebarikiwa ardhi yenye rutuba na mvua za kutosha zinazowasaidia uzalishaji wa mazao mbalimbali kama tangawizi, mihogo ndizi, maharage n.k ila ukosefu wa pembejeo na wataalam wa kilimo kupelekea kutokupata matokeo mazuri kipindi cha mavuno.
Screenshot_20250418-153718.jpg

Hii ni picha ya satellite ya kijiji cha Lumbiji.

Zifuatazo ni picha mbalimbali nilizozipata kwa kamera yangu na changamoto tulizopitia mpaka kufika kijijini hapa ningependa kushare nanyi÷

IMG_20250415_174647.jpg

IMG_20250415_174634.jpg

Tulijiandaa na safari vizuri mimi na rafiki yangu ambaye ni classmate wangu wa O-level huko ndiko asili yake ilipo mimi nipo kwenye utalii wa ndani tu.
IMG_20240109_144010-01.jpeg

IMG_20240109_144046-01.jpeg

Hizi picha tulipiga tulipoiacha barabara kuu ya lami ya kuelekea wilayani Kilosa inayotokea Dumila Morogoro hapo tulikuwa na safari ya zaidi ya km 50 juu milimani kukifikia kijiji cha Lumbiji.

IMG_20240109_164247-01.jpeg

IMG_20240109_164156-01.jpeg

Hizi picha tulipiga baada ya kuwasili kijijini hapo ilikuwa safari kama ya masaa 2 kuanzia tulipo iacha lami ila imebeba historia mpya maishani mwangu.

Kuna njia(barabara) hatari ambazo sijawahi kukutana nazo tangu kuzaliwa kwangu hii experience mpya imeniongezea ujasiri pia nimepata funzo kwenye maisha.

HITIMISHO
Kuanzia leo nimeanzisha kampeni ya kuchangisha mchango utakaowezesha kupika chakula cha pamoja na kula na watoto katika sikukuu ya pasaka ili kuwaonyesha upendo na kuwafanya siku yao kuwa na tofauti na siku.
Watoto wengi wana changamoto ya mavazi ila binafsi sina uwezo wa kuwasaidia mmoja mmoja kwa wingi wao ndio maana nimekuja na hili la kuandaa chakula cha pamoja kutokana na fani yangu ya upishi ningependa wapate taste ya tofauti katika sikukuu hii ya Pasaka na tujifunze mambo mbalimbali pamoja.

KAMA UTAPENDA KUCHANGIA MLO WA WATOTO WA SIKUKUU HII YA PASAKA NAWEKA ACCOUNTS ZANGU PIA NITAAGIZA VIFAA VYA SHULE MJINI KADRI MUNGU ATAKAVYOKUWA AMUTUJAALIA.
 
View attachment 3308604
Hii ni picha ya satellite ya kijiji cha Lumbiji.

Zifuatazo ni picha mbalimbali nilizozipata kwa kamera yangu na changamoto tulizopitia mpaka kufika kijijini hapa ningependa kushare nanyi÷

View attachment 3308607
View attachment 3308609
Tulijiandaa na safari vizuri mimi na rafiki yangu ambaye ni classmate wangu wa O-level huko ndiko asili yake ilipo mimi nipo kwenye utalii wa ndani tu.
View attachment 3308619
View attachment 3308620
Hizi picha tulipiga tulipoiacha barabara kuu ya lami ya kuelekea wilayani Kilosa inayotokea Dumila Morogoro hapo tulikuwa na safari ya zaidi ya km 50 juu milimani kukifikia kijiji cha Lumbiji.

View attachment 3308627
View attachment 3308628
Hizi picha tulipiga baada ya kuwasili kijijini hapo ilikuwa safari kama ya masaa 2 kuanzia tulipo iacha lami ila imebeba historia mpya maishani mwangu.
Kuna njia(barabara) hatari ambazo sijawahi kukutana nazo tangu kuzaliwa kwangu hii experience mpya imeniongezea ujasiri pia nimepata funzo kwenye maisha.

HITIMISHO
Kuanzia leo nimeanzisha kampeni ya kuchangisha mchango utakaowezesha kupika chakula cha pamoja na kula na watoto katika sikukuu ya pasaka ili kuwaonyesha upendo na kuwafanya siku yao kuwa na tofauti na siku.
Watoto wengi wana changamoto ya mavazi ila binafsi sina uwezo wa kuwasaidia mmoja mmoja kwa wingi wao ndio maana nimekuja na hili la kuandaa chakula cha pamoja kutokana na fani yangu ya upishi ningependa wapate taste ya tofauti katika sikukuu hii ya Pasaka na tujifunze mambo mbalimbali pamoja.

KAMA UTAPENDA KUCHANGIA MLO WA WATOTO WA SIKUKUU HII YA PASAKA NAWEKA ACCOUNTS ZANGU PIA NITAAGIZA VIFAA VYA SHULE MJINI KADRI MUNGU ATAKAVYOKUWA AMUTUJAALIA.

MIXX BY YAS - 0679756348
JINA : GERALD NKALALWE

CRDB - 0152699086700
JINA : GERALD NKALALWE

KWA PAMOJA TUNAWEZA KUWA SEHEMU YA MABADILIKO KATIKA JAMII.
Wazo zuri!
 
Nashukuru ndugu zangu Mungu awabariki michango yenu kwa ajili ya watoto nimeiona naamini watakuwa na siku yenye neema.
 
Back
Top Bottom