Pan African Movement of East and Central Africa (PAFMECA)

Pan African Movement of East and Central Africa (PAFMECA)

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
MKUTANO WA PAFMECA MOSHI 1959

Kanirushia ndugu yangu barua hii ya PAFMECA nami nimeiweka hapa sote tufaidi.

Naweka hapo chini kipande kidogo kuhusu PAFMECA kutoka kitabu cha Abdul Sykes:

Pan African Movement of East and Central Africa (PAFMECA), 1958

''Ilikuwa katika ya mazingira ya namna hii na uhusiano mzuri kati ya TANU na KANU ndiyo Nyerere alisafiri kwenda Nairobi kukutana na Tom Mboya.

Uamuzi ulitolewa kuunda umoja ili kuunganisha vyama vyote vya kupigania uhuru katika Afrika ya Mashariki - Pan-African Movement of East Africa (PAFMECA).

Chama hiki kiliundwa rasmi mjini Mwanza na wawakilishi wa vyama vya kizalendo kutoka Tanganyika, Zanzibar, Kenya, Uganda na Nyasaland mnamo tarehe 17 Septemba, 1958.

Tanganyika ilipewa heshima hiyo kwa sababu chama chake cha kizalendo, TANU kilikuwa ndicho chama kilichokuwa kikiendeshwa kwa ufanisi zaidi na chenye nguvu sana kuliko vyama vyote katika kanda ile.

TANU ilikuwa imeweza kujenga amani na umoja katika chama. Mizozo ndani ya chama haikuwepo.

TANU kilikuwa chama cha siasa cha kupigiwa mfano katika Afrika.

Bhoke Munanka alichaguliwa rasmi kuongoza ofisi ya PAFMECA katika makao makuu ya TANU.''

1674619527112.png
 
Enzi hizo mambo ya shilingi moja na senti hamsini dah kweli Mda unaenda sana
 
Back
Top Bottom