Pancha kwenye upande wa tairi

Haifai kabisa. Huwa inakauka na kujikusanya sehemu moja. Inaharibu wheel balance. Ukiwa safari gari litakuboa aise. Hayo madude hayafai.
Ni kweli kabisa mkuu, zinafaa tu kwenye tair za pikipiki tena iwe imeanza kuchoka, ukiweka kwenye tair mpya ujue ushaiua,

Hii dawa ingekuwa nzur bac kila mtu angeweka maana hakuna anaependa kupata pancha wakati OKO ipo ukitia inazibaaa....mwanzon watu waliishobokea ila baada ya kujua madhara yake walikimbia chap kwa haraka
 
Kabisa. Maana enzi hizo kila ukienda kuziba tairi jamaa lazima warecommend.
 
wataalamu wanasema viraka vya pembeni ya tairi havifai kwa sababu tairi ikipungua upepo kiraka cha pembeni kinatabia ya kulegea na kutoka hii inatokana na kuwa airi likpungua upepo linatabia ya kulegea

wanashauri kiraka kiwekwe juu ya tairi(ile sehemu ambayo tairi linakanyaga chuni_) wanasema pale kiraka kinakandamizwa na sio rahisi kubanduka

pembeni ya tairi unatakiwa kuziba na utambi na sio kiraka

ila kwa mwenye elimu zaid aje atuelimishe wana jukwaa

nko tayari kukosoleewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…