Pande mbili: Yaani Serikali na CHADEMA, vitafakari Kwa makini, athari zitazotokea, iwapo maandamano hayo yaliyoandaliwa na CHADEMA yatafanyika

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,843
Reaction score
31,057
Hadi sasa inaelekea Kuna mvutano mkubwa Kati ya serikali na CHADEMA, kuhusu maandamano ya amani, yaliyopangwa na CHADEMA tarehe 23 mwezi huu, kama serikali itakuwa haijatoa taarifa yoyote kuhusu kifo Cha kiongozi wao Ali Kibao na haitaeleza walipo viongozi wao wa vijana, akina Deusdedit Soka na wenzake wawili, ifikapo tarehe 21 mwezi huu.

Kwa hali ninayoiona kutokana na hotuba iliyotolewa na Rais Samia, katika sherehe za kuadhimisha miaka 60, tangu Jeshi hilo lianzishwe, dalili ni finyu sana kufikiwa muafaka wa suala Hilo.

Rais Samia alitoa msimamo wa serikali yake kuwa, haiwezi kuelekezwa Cha kufanya na mabalozi wa nchi za nje, viongozi wa vyama vya upinzani hapa nchini na viongozi mbalimbali wa dini, walioiomba serikali, iunde Tume huru ya kuchunguza Kwa visa hivyo vya kutekana na baadhi ya wahanga hao kuuliwa.

Ingawa Kila upande unavutia upande wake, Kwa upande wa serikali, ukionya vikali kuwa maandamano hayo imeyapiga marufuku, wakati chama Cha CHADEMA kikidai kuwa maandamano hayo yapo pale pale, kama yaliyopangwa, Kwa sababu serikali haijatoa majibu Kwa masuala iliyoyauliza.

Ni wazi kuwa kutokana na mtifuano huo mkali, nchi yetu ipo njia panda ya kuelekea Kwenye machafuko ya umwagikaji wa damu, iwapo CHADEMA watatekeleza kuingia Kwenye maandamano hayo kama walivyopanga.

Nianze Kwa upande wa serikali, ni lazima itafakari Kwa makini kuyapiga marufuku maandamano hayo ya amani yaliyoratibiwa na CHADEMA, kuhusu athari itakazozipata iwapo itatekeleza azma yao ya kuyavunja maandamano hayo, hata kama ni Kwa kutumia nguvu.

Kwanza, ni jambo inalosikitisha na linaloonyesha wazi kuwa serikali hii, imepuuza, madai yote ya CHADEMA, Jumuia ya Kimataifa, viongozi wakuu wa dini mbalimbali, pomoja na wanaharakati mbalimbali, waliotaka serikali iunde Tume huru ya uchunguzi, Ili ibainike wahusika wa vitendo hivyo viovu.

Ifahamike pia kuwa Jumuia ya kimataifa itakuwa macho, kuangalia matokeo ya maandamano hayo, Kwa kuwa na wao ni miongoni waliotoa wito Kwa serikali hii Ili iunde Tume huru ya uchunguzi.

Kwa maana hiyo, iwapo maafa yatatokea Kwenye maandamano hayo, watatoa ripoti Kwenye nchi zao na hivyo picha ya nchi yetu kimataifa, itakuwa imeharibika mno na ipo hatari, misaada na mikopo mbalimbali ambayo nchi yetu imekuwa ikipata kutoka Kwenye nchi hizo, itakuwa ndiyo mwisho wa kuipata!

Nije Kwa upande wa CHADEMA, ingawa wao Wana haki zote za kuandaa maandamano hayo ya amani, kutokana na wao kuona kuwa hawatendewi haki na hata Katiba ya nchi yetu inaruhusu kifanyika Kwa maandamano hayo na njia pekee, wanayoona wao iliyosalia ni kufanya maandamano hayo ya amani.

Hata hivyo naomba pia kuwatahafharisha CHADEMA kuwa na wao wanapaswa kutafakari Kwa makini, kama maandamano hayo yafanyike au laa, Kwa kuwa serikali hii imeshatangaza kibabe bila kutumia sheria yoyote ya kuyafuta maandamano hayo, sasa ukizingatia kuwa askari hao watakuja Kwa nia ya kupambana na waandamaji hao, ni dhahiri maafa yanaweza kutokea.

Kwa hiyo niwasihi wana-CHADEMA nao walizingatie Hilo Kwa umakini mkubwa.

Mungu ibariki Tanzania
 
..bado ACT hawajambana bwana mdogo kisawasawa, lakini na kwenyewe kitanuka karibuni. Kule uchaguzi huwa haufanyiki bila mauaji ya wapinzani.
Atatumia jeshi letu la Tanganyika, maza ni mjanja sn kwao hana tatizo shida ake ni huku kwetu anataka tugombane yeye arudi kwao ambako amepajenga kwa pesa za wabara
 
Tatizo ni la Watanganyika wamezidi uchawa ndio wanampa kichwa.

Kule kwao hawawezi kukubali kuongozwa na mwanamke kwanza dini tu hairuhusu utashangaa baraza la Idd machawa ya Bakwata eti mgeni rasmi mwanamke.
Yap wanampa kichwa haswa, chawa wanafaidi kuiba mali za umma bila kukamatwa ndiyo maana
 
Turejee kwenye sheria.

Kuadamana na kukusanyika ni haki za msingi kwa kila mtu, hizi ni haki ambazo zimeruuhusiwa kwa mujibu wa sheria za ndani Pamoja na sheria za kimataifa ambazo Tanzania imezisaini.

Miongoni mwa sheria hizo za kimataifa ni:-
Tamko la kimataifa la haki za binadamu la mwaka (1948).

Mkataba wa kiafrika wahaki za binadamu na haki za watu wa mwaka (1981) na

Mkataba wa haki zakisiasa na kiraia wa mwaka (1966)

Kwa mujibu wa sheria za ndani ni Pamoja na
katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania yamwaka (1977) sura ya pili imeeleza wazi kuwa kuandamana ni haki ya msingi ya raia

Chadema wamesema watafanya mandamano ya AMANI na ni haki yao kisheria kama nilivyo eleza hapo mwanzo, jukumu la serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama specifically jeshi la polisi ni kutoa ulinzi kwa wandamanji na kama kuna viashiria vya fujo au uvunjifu wa amani basi wawakamate hao wanaopanga kuleta hizo fujo kwasababu ninamini intelejensia inafanya kazi vizuri

Vinginevyo watoe majibu ya maswali ya Chadema kuhusu kupotea na kuuwawa kwa watu wao, kwa sababu kama serikali ingetoa majibu sambamba na kuwafikisha mahakamani waliohusika na tuhuma izo basi binafsi ninaamini kusingekuwepo hayo maandamano.
 
Umefafanua vyema sana👋👋
 
Eh kumbe maandamano yameandaliwa na Chadema, nikajua yameandaliwa na wananchi.

Hakuna maandamano ya kuipinga serikali yanayoanzishwa na chama pinzani yakafanikiwa.
 
Hakuna ya smani wala nini, POLISI washasema MARIFUKU.
 
Kwa hali ninayoiona kutokana na hotuba iliyotolewa na Rais Samia, katika sherehe za kuadhimisha miaka 60, tangu Jeshi hilo lianzishwe, dalili ni finyu sana kufikiwa muafaka wa suala Hilo.
Mzee Lipumba ameomba Polisi waache upumbavu wakae wawasikilize CHADEMA. Polisi walivyowajinga wanashupaza shingo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…