kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Hii panga pangua ya mama kuhusu mashirika ya umma inatia shaka. Kwanza tujiulize ni mashirika gani ya biashara yanaendeshwa na serikali. Mengi yalikwisha binafsishwa zamani kabisa enzi ya mkapa.
Kwenye hii awamu binafsi naona ni wapiga dili watupu. Mashirika mengi yaliyobakia serikalini yale ya kudhibiti 'regulatory' bodies sasa unayatishia kubinafsisha au kuyaacha yafe kama hayawezi kujitegemee wakati yenyewe yanafanya kazi za kiserikali tu?
Kuna maeneo tuliona hatuwezi kuachia sekta binafsi kwa sababu yanahusika na uhuru wetu au ni muhimu lakini hakuna muwekezaji anataka kubeba hiyo risk. Sasa serikali ikija na lawama kwamba shirika kama TPDC eti litaachiwa life kama haliwezi kujiendesha hiyo ni akili gani. Hapo sikutaka kufifisha harakati za kutafuta mafuta na gesi au kudhibiti uingizaji wa mafuta nchini? Ukiangalia shirika kama TTCL ni shirika muhimu sana kwa umma lakini makampuni binafsi yanataka life ili kusiwe na uwekezaji wa umma kwenye eneo hilo. Tuliona awamu ya tano juhudi ya kuimarisha ttcl na stamico hata kulikomboa shirika la ttcl kwenye ubinafsishaji bandia na kukomboa hisa zake kwenye airtel zilizokua zimeporwa.
Ajabu ni kutishiwa TTCL kutelekezwa ife kama haiwezi eti kujiendesha. Tunajua kila wakati ttcl kwenye ushindani inakuja na vifurushi vya bei ya chini waziri wa sasa Nape amekua akiingilia eti wapandishe kwa kua ushindani wao sio fair kwa kampuni zingine za simu. Huo ni uingiliaji wa ajabu sana kwa waziri. Ukienda huko hazina unakuta msajili wa mashirika na hisa za serikali kwenye mashirika mtu alitemwa na jpm samia kamrudisha. Kwa kweli ni mashaka matupu.
Hili la kufikiri sekta binafsi ndio ya kuachiwa kila kitu ni hatari sana. Sekta binafsi wanaweza kujijali wao tu lakini sio kufanya kazi ya kuendeleza nchi. Kwanza sekta binafsi yetu bado ni kama mawakala tu wa biashara kubwa kimataifa. Serikali isikwepe majukumu yake kwa lengo la ubinafsi wa watendaji wake kama wanavyotaka kufanya kwa bandari.