Panga pangua ya mashirika ya umma hebu tuangalie kwa darubini

Tatizo la mashirika ya serikali ni kuwa wafanyakazi wa hayo mashirika ni wafanyakazi wa serikali...

Yatakiwa mashirika yajiendeshe kwa pesa yao, yakipata hasara yapunguze wafanyakazi
Tatizo linaanzia juu kwenye uongozi.

Wakurugenzi na hizi bodi za wakurugenzi za haya mashirika haziko competetive, hazina ubunifu na wanatumiwa vibaya na wanasiasa na wafanyabishara wakubwa

Ukienda private sector ukiona kampuni inafanya vizuri angalia management lazima utakuta iko vizuri kwenye kusimamia na kuongoza mambo

 
Sababu hakuna permanent jobs.
Wafanyakazi wa serikali wakishapata kazi wao ni kwenda kusign na kupiga porojo.
Wafanyakazi wrngi wa serikali ambao ofisi zao hazina attendance register ya umeme hutumia wenzao kusaini
 
Na wengi ni vilaza na walamba ma.kalio🤣ashakum si matusi
Hizo nafasi wamezipata kwa kujikombakomba sana
Huwezi ona utendaji(performance) kwa mtu kama huyo🙏
 
Sababu hakuna permanent jobs.
Wafanyakazi wa serikali wakishapata kazi wao ni kwenda kusign na kupiga porojo.
Wafanyakazi wrngi wa serikali ambao ofisi zao hazina attendance register ya umeme hutumia wenzao kusaini
Attendance register za umeme ziko nchi nzima,wanaziua tu
Huku niliko Ina mwaka na nusu ilipiga shot,na haijawahi rekebishwa
Kifupi habari iliishia hapo🤣🤣
 
Kuna akili za kiafrika, kitanzania, kikanda, kimataifa, Watanzania hasa viongozi kwenye eneo la siasa hawana akili maridhawa na ambazo ni mtambuka. Any kind of thinking in any case has to be contextualized on suitability, relevance, validity, we have infant states with everything being infant, you can't bring Things or models from western world foolishly, look at structures, maturity, critical thinking and analysis, moral, constitutionality, democracy state. Rule of law. Institutional autonomy. Gradual transformation, with closer review, monitoring and evaluation, transformation with hybridization in the process is very vital.
 
Attendance register za umeme ziko nchi nzima,wanaziua tu
Huku niliko Ina mwaka na nusu ilipiga shot,na haijawahi rekebishwa
Kifupi habari iliishia hapo[emoji1787][emoji1787]
Tatizo ni tamisemi

Ili watu wafanye kazi vizuri waondoe kipengele cha ajira ya kudumu, watu wapewe mkataba wa miaka 5 renewable
 
Naona vyeo vinaenda kupotea umekuja kujitetea huku.

Ni hivi Rais Samia sio mtu wa kubeba wajinga,kama mlikubaliana mlete faida lazima ionekane mezani,huwezi pisha na mbaya zaidi mtaanza kuomba kazi nyie ma CEO.

No more inefficiency awamu ya 6
 
Una upeo mkubwa sana chief
 
Akili kubwa hii.

Ni kama umekazia kwamba kazi ya uongozi yaani regulation ibaki kuwa kazi ya serikali. Na ndiyo serikali hata kwa tafsiri ghafi tu.

Labda tatizo ni pale ambapo wafanyakazi tuliowaweka kama serikali, ili wafanye kazi ya uongozi na usimamizi wanaposhindwa kufanya kazi zao kikamilifu.

Kimsingi inatakiwa tu kila mtu awe ni, kile anachojinasibu kuwa yeye ni;
Mkaguzi afanye ukaguzi
Msimamia sheria aisimamie
Mpokea ripoti afanyie kazi
Na muwajibishaji awe na men.... no ayatumie meno yake barabara
 
Kuna udhaifu wa usimamizi upande wa serikali. Solution ni kuja serikali nyingine sio kuua taasisi au kampuni za umma.
 
Hayo mashirika pia kuyabinafsisha ni Kumcompromise na National Security, Wapigaji wao hawalioni ilo kabisa wanawaza ulaji tu Shirika kama tanesco ni giant one na wameshanusa budget zake na Operations zake wameona kuna Pesa
 
Sababu hakuna permanent jobs.
Wafanyakazi wa serikali wakishapata kazi wao ni kwenda kusign na kupiga porojo.
Wafanyakazi wrngi wa serikali ambao ofisi zao hazina attendance register ya umeme hutumia wenzao kusaini
Maboss na wasimamizi ndio wa kudeal nao wakinyooshwa hao watawanyoosha wa chini.

Kuwa mfanyakazi wa serikali sio kigezo cha kuhalisha kutofanya kazi kwa weledi

Usimamizi mbovu wa wakubwa katika maeneo ya kazi ndiyo chanzo cha uzembe.

Ndio maana kila shirika na taasisi za serikali kuna uongozi hawa ikiwa wanafanya kazi yao ya kuwaongoza wafanyakazi wafanye kazi kwa weledi tungeona ufanisi


Niliwahi kufanya kazi benki fulani bodi ya wakurugenzi walimpandisha cheo jamaa nafasi ya Director of Business Banking and Small Medium Enterprises baada ya aliyekuwepo kuondoka

Wakampa malengo aliyopaswa ayafikie ndani ya kipindi fulani cha wakati aliposhindwa wakamshusha cheo akarudi alipokuwa akaletwa jamaa mpya akayafikia malengo

Serikali itumie huo mfumo kwenye mashirika ya umma mkurugenzi na bodi yake wawekewe malengo wasipoyafikia shusha vyeo na kama wameiba tupa jela. Wakibanwa hawa watafanya juu chini walio chini yao wafanye kazi kwa weledi. Hii itapunguza mazoea kwenye utendaji.

Tutake tusitake lazima kuna mashirika na huduma ziwe chini ya serikali kwa sababu za kiusalama na huduma nyeti na muhimu wanazotoa. Hata ukienda nchi zenye mfumo wa capitalism kama Marekani na za Ulaya kuna huduma zinatolewa na mashirika yaliyo chini ya serikali tu
 
Cha kujiuliza je hayo mashirika yana umuhimu au hayana. Na kama yalianzishisha kwa lengo mahsusi je si makosa ya uongozi kushindwa kuyadimamia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…