"Panya" - alitolewa kwa helikopta na kusafirishwa hadi mji mkuu.

"Panya" - alitolewa kwa helikopta na kusafirishwa hadi mji mkuu.

IamBrianLeeSnr

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2022
Posts
2,010
Reaction score
4,179
KWELI DUNIANI WATU WAWILI-WAWILI...
BD4685ED-A8D6-4B71-AEC4-BCCD5C427C44.jpeg

Jamaa huyo ambaye ni moja ya cast kwenye series ya MONEY HEIST anaefahamika kwa jina la Denver anaonekana kufanana au mwenye mwonekano unaofanana na OVIDIO GUZMAN the son of JOAQUIN EL CHAPO

Tetesi hizi za kufanana kwa wawili hao zimechipuka na kuanza kuzungumzwa na baadhi ya watu ulimwenguni baada ya mtoto wa muuzaji wa madawa ya kulevya, Joaquín "El Chapo" kukamatwa na kikosi cha askari polisi wa NEW YORK POLICE DEPARTMENT FORCE (NYPD)

Ovidio Guzmán-López, 32, anayedaiwa kuwa kiongozi wa genge la zamani la babake, alikamatwa huko Culiacán na kusafirishwa hadi Mexico City siku ya Alhamisi.

Lakini wakati na baada ya kukamatwa, askari 10 na washukiwa 19 waliuawa.
Washiriki wa genge wenye hasira waliweka vizuizi barabarani, wakachoma moto makumi ya magari na kushambulia ndege katika uwanja wa ndege wa eneo hilo.

Wanajeshi wengine 35 walijeruhiwa na watu 21 wenye silaha walikamatwa, Waziri wa Ulinzi Luis Cresencio Sandoval alisema Ijumaa.

Bw Guzmán-López - aliyepewa jina la utani "Panya" - alitolewa kwa helikopta na kusafirishwa hadi mji mkuu kabla ya kupelekwa katika gereza la shirikisho lenye ulinzi mkali.

Anashutumiwa kwa kuongoza kundi la babake maarufu la Sinaloa – mojawapo ya mashirika makubwa zaidi ya ulanguzi wa dawa za kulevya duniani.

Babake, Joaquín "El Chapo" Guzmán, anatumikia kifungo cha maisha jela nchini Marekani baada ya kupatikana na hatia mwaka wa 2019 ya ulanguzi wa dawa za kulevya na utakatishaji fedha. Kesi yake ilifichua baadhi ya maelezo ya kikatili ya jinsi mashirika ya dawa za kulevya nchini Mexico yanavyofanya kazi.
 
Ismail Zambada aka El- Mayo ndio bosi pekee aliyebaki wa Sinaloa Cartel, baada ya kukamatwa kwake juzi kati na yule dogo mwingine wa Elchapo pale niliamini ulikuwa mwisho wa Sinaloa Cartel na mamlaka zimeamua sasa, hawa wengine walikuwa bado hawajakomaa kwenye game.

El-Mayo alikuwa low key sana.

Kwasasa wale wahuni wengine wa CJNG watakuwa moto sana.
Haya makundi yamekuwa na nguvu sana miaka na miaka mpaka kuizidi nguvu serikali ya Mexico.
 
Back
Top Bottom