Papa alipotembelea Moshi!!!

Papa alipotembelea Moshi!!!

Lole Gwakisa

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2008
Posts
4,768
Reaction score
2,361
Papa aliamua kutembelea sehemu za Moshi kwa ibada maalum baada ya kuambiwa Moshi kuna wakristo wengi sana.
Na kweli, kufika pale Moshi ibada ilifanyika uwanja wa wazi na watu weeengi sana walifurika uwanjani,wakubwa kwa watoto, wake kwa waume.
Papa alishangaa sana kuona umati ule na akavutiwa maana hata machifu walikuwepo, Marealle,Massawe, Moshi, Mushi, Mwasha na hata Kimaro na Kimario.
Papa akwaona wazee wa pale Moshi na kuwauliza, "hawa watu niwaombee nini toka kwa Baba aliyeko juu?"
Baada ya majadiliano mafupi na waumini wao wazee wale wakamjibu Papa.
Ombi kubwa wanaloomba lifutwe na linawakwaza sana ni amri ya saba, USIIBE.
Masikini Papa akazimia!
 
watu wa moshi sio wezi bwana, ni wajasiliamali wanaodhubutu!!
 
Papa alipofika New York City, muandishi mmoja wa gazeti la kidaku la "New York Post" alijipenyeza mpaka kumfikia karibu naye na kumuuliza "Baba Mtakatifu, unajua kwamba hapa New York kuna malaya wanaojiuza karibu sehemu zote za mji ?" Papa huku akifikiri kwa huruma akamjibu kwa kuuliza swali lile lile "Hivi hapa New York kuna malaya ?"

Kesho yake gazeti likatoa headline kubwa.

Papa auliza "New York kuna Malaya?"
 
ha ha ha, mie mchagga bwana:smile-big:
 
Papa mwenyewe mchagga wa kishumundu wallah nakwambia.
Aikambe
 
Back
Top Bottom