Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Dunaini, Papa Francis, amelaani kwa matamshi makali vitendo vya kuchomwa kitabu kitakatifu kwa Waislamu, Qur'an.
Papa Francis pia ametoa wito wa kuheshimiwa kwa vitabu vitakatifu vya dini kama njla ya kuonesha heshima kwa Watu wanaoviamini, katika mahojiano na gazeti la Al-Ittihad linalochapishwa huko Falme za Kiarabu, Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki amesema amechukizwa na matendo hayo na kupinga juhudi zozote za kuruhusu matukio hayo kuwa sehemu ya uhuru wa maoni.
Kauli ya Papa Francis inakuja kufuatia kitendo cha wiki iliyopita ambapo Mtu mmoja alichoma Quran Tukufu kwenye Miji mkuu wa Sweden, Stockholm, na kuibua hasira kutoka Mataifa kadhaa duniani.
Ingawa Mamlaka za Sweden zimekuwa zikikataa maombi ya maandamano ya kuipinga Quran, Mahakama za nchi hiyo zimepinga katazo hilo zikisema zinaingilia uhuru wa Watu kujieleza.
Chanzo: Millard Ayo