SI KWELI Papa Francis amefariki leo, Februari 24, 2024

SI KWELI Papa Francis amefariki leo, Februari 24, 2024

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Je hii ni kweli?
1740395429553.png

1740395449989.png
 
Tunachokijua
Papa Francis ni kiongozi wa kanisa katoliki duniani ambaye alichaguliwa katika nafasi hiyo mnamo tarehe 13 Machi 2013.

Mnamo tarehe 14 Februari 2025, Papa Francis alilazwa katika hospitali ya Agostino Gemelli, Roma ambapo alifanya vipimo vya kitaalam na kuanza matibabu ya dawa baada ya vipimo vya kwanza kuonesha kuwa ana maambukizi kwenye njia ya upumuaji.

Februari 23, 2025 Ofisi ya Habari ya Vyombo vya habari Vatican ilitoa taarifa kuhusu matibabu ya Baba Mtakatifu Francisko, ikisema
"Hali ya Baba Mtakatifu bado ni tete, lakini tangu jana jioni, hajapata matatizo zaidi ya kupumua. Alifanyiwa vipimo viwili vya seli nyekundu za damu zilizojilimbikizia na matokeo ya vipimo vyake vya damu vimeongezeka."

Kumekuwapo taarifa ambazo zimekuwa zikisambazwa katika mitandao ya kijamii zikidai kuwa Papa Francis amefariki kutokana na muendelezo wa taarifa za kuumwa kwake.


Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck ulibaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani Papa Francis yupo hai na anaendelea na matibabu katika hospitali ya Agostino Gemelli, Roma. Hakuna chanzo cha kuaminika kilichochapisha taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Vatican News Jumatatu Februari 24, 2025 ikirelea ofisi ya habari ya Vatican iliyobainisha hali ya maendeleo ya afya ya Papa, ilisema "Usiku ulienda vizuri; Papa amelala na anapumzika," Jioni ya Jumapili, Ofisi ya Habari ya Vatican ilisema hali yake bado ni mahututi, ingawa hajapata matatizo ya kupumua tangu asubuhi ya Jumamosi. Kadhalika Papa Francisko aliongezewa damu ili kuongeza kiwango cha hemoglobini mwilini mwake huku baadhi ya vipimo vya damu vikionesha dalili za kufeli kwa figo.
papa-francesco.jpg
Kuna siku uliniwakia ikabidi niwe mpole tu..
Shida nyie binadamu mtu akiwa mpole mpole mnaweza hata kumbaka sasa usipojipindua akili huachwi salama!, just imagine unabakwa na mdada...🤣
 
Bora afe tu maana Hana mamlaka ya kimungu Kwa sababu Kawa na kigugumizi kuukemea shoga
 
Back
Top Bottom