Papa Francis atuma salamu za rambirambi kufuatia ajali ya Precision Air

Papa Francis atuma salamu za rambirambi kufuatia ajali ya Precision Air

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Katibu Mkuu wa Vatican, Kadinali Pietro Parolin, kwa niaba ya Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis ametuma salamu za rambirambi kwa watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia ajali mbaya ya ndege ya Precision Air iliyosababisha watu 19 wapoteze uhai.

Papa Francis ametoa hakikisho la kuwa karibu kiroho kupitia sala kwa watu wote waliokumbwa na mkasa huu hasa kwa familia na wahanga wote.

Anaziombea roho za marehemu zipate pumziko la milele, majeruhi wapone haraka na anawaombea wajazwe nguvu wote wanaohusika kwenye uokozi na matibabu ya majeruhi.

Zaidi ya yote, Papa anaomba faraja na amani ya Mwenyezi Mungu itawale kwa ndugu jamaa na marafiki wote waliokumbwa msiba huo mkubwa.

B4F516A2-4E00-4881-9479-F13ED17275C6.jpeg
 
Ana unafiki huyu mbona ajali kibao huwa zinatokea za mabasi nchini. Hata Ile ajali ya mtwara ya wanafunzi.
 
Back
Top Bottom