Papa Francis: Suluhu ya amani ipatikane Niger

Kingsmann

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2018
Posts
4,805
Reaction score
17,850
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis ameelezea matumaini yake ya kupatikana kwa suluhu ya amani katika mgogoro wa Niger kufuatia mapinduzi ya Rais yaliyofanyika katika Taifa hilo la Afrika Magharibi.

DW Kiswahili imeripoti kuwa Papa amewaambia Waumini katika uwanja wa St Peters kwamba anafuatilia matukio hayo kwa wasiwasi akiunga mkono ombi la kuwa na amani nchini humo na udhabiti katika Kanda nzima ya Sahel.

Ametoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kupata suluhusu ya amani haraka iwezekanavyo katika mzozo huo kwa manufaa ya Wananchi wa Niger.

Mwezi uliopita, Kiongozi wa utawala wa kijeshi Abdourahamane Tchiani, alimpindua Rais aliyechaguliwa kidemokrasia Mohamed Bazoum, hadi sasa Bazoum, Mkewe na Mtoto wake wa kiume wamewekwa katika kifungo cha nyumbani katika Mji mkuu wa Niger uitwao Niamey.

20230821_115046.jpg

Source: Millardayo
 
View attachment 2723774

Source: Millardayo
Tunamsubiri kikwete atoe neno na hapa
 
Back
Top Bottom