SI KWELI Papa hawapati saratani hivyo wanaweza kutumika kama tiba ya saratani?

SI KWELI Papa hawapati saratani hivyo wanaweza kutumika kama tiba ya saratani?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kumekuwa na taarifa kuwa samaki aina ya Papa ana uwezo wa kuzuia saratani na anaweza kutumika kama tiba ya saratani. Ni upi uhalisia wake?
1787125863879.png
 
Tunachokijua
Papa ni samaki wa baharini wenye sifa za kipekee za kibaolojia. kuna zaidi ya spishi 400 za papa duniani, na mifupa yao imeundwa kwa gegedu (cartilage) badala ya mifupa. papa wana jeni zinazosaidia kuzuia uharibifu wa DNA.

Madai


Kumekuwa na madai kuwa Papa hawapati saratani, hivyo wanaweza kutumika kama tiba ya saratani. Dai hili limeenea kwa muda mrefu, hasa kutokana na imani kwamba papa wana kinga dhidi ya saratani.

Makala iliyochapishwa na Shark Stewards inaeleza kwamba dhana hiyo ilienezwa sana kupitia kitabu cha mwaka 1992 cha "Sharks Don’t Get Cancer", ambacho kilitumika kukuza shark cartilage kama tiba ya saratani.

Uhalisia


Ufuatilia umebaini kuwa dai hili si la kweli, ukweli ni kwamba papa wanaweza kupata saratani. The Tech Interactive inaeleza kwamba imani kwamba papa hawapati saratani ni dhana potofu na kwamba tayari kumekuwa na visa vingi vya papa wenye saratani ama uvimbe.

Makala iliyochapishwa na Shark Stewards inaongeza kwamba wataalamu wameonyesha kuwa papa wanaweza kupata uvimbe usio wa saratani na uvimbe wa saratani. Kulingana na makala hiyo, kumbukumbu za uvimbe katika papa, skate na rays zimekuwepo tangu mwaka 1908, zikiwemo melanoma na carcinomas.

Ni kweli kwamba papa wana mifumo ya kibaolojia inayosaidia kuzuia mabadiliko, na watafiti wanaamini kujifunza mifumo hiyo kunaweza kutoa mawazo mapya katika utafiti wa saratani kwa binadamu. Hata hivyo, hilo halimaanishi kwamba papa hawawezi kupata saratani.

Vilevile, shark cartilage haijaonyeshwa kisayansi kupambana na saratani kwa binadamu. The Tech Interactive inaeleza kwamba tafiti za kitabibu hazijaonyesha kuwa shark cartilage inaweza kupambana na saratani kwa binadamu.

Shark Stewards pia inasema wazi kwamba kutumia shark cartilage hakutibu saratani kwa binadamu. Kwa hiyo, ukweli kwamba papa wana cartilage na baadhi ya sifa zinazowavutia watafiti hauwezi kutumiwa kuthibitisha kwamba sehemu za papa ni dawa ya saratani. Papa wanaweza kupata saratani, ingawa wana mifumo ya kipekee ya kibaolojia inayowavutia watafiti.
Back
Top Bottom