Papa Leo XIV amteua Padri Monsinyori Romanus Mbena kuwa mkuu wa huduma ya Upendo Vatican

Inside10

Platinum Member
Joined
May 20, 2011
Posts
34,776
Reaction score
42,933

Baba Mtakatifu Leo XIV amemteuwa mtanzania Monsinyori Romanus Mbena kuwa ni Mkuu wa Ofisi ya Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo, ambaye hadi kuteuliwa kwake amekuwa akihudumu kama Afisa Mshauri wa Balozi za Vatican ngazi ya kwanza na Mhudumu katika masuala ya jumla kwenye Sekretarieti kuu ya Vatican. Monsinyori Romanus Mbena alipadrishwa mwaka 1992 Jimbo Katoliki la Morogoro na kuanza utume wake katika Diplomasia mwaka 1995.

- Baraza hili liko chini ya Mtunzaji mkuu wa Sadaka ya Kipapa anayeshirikiana na Mabaraza mengine, ili kuhakikisha kwamba, misaada inawafikia walengwa, kutoka kwa Khalifa wa Mtakatifu Petro, Mchungaji mkuu wa Kanisa la Kiulimwengu kwa ajili ya maskini, watu wanaosukumiziwa pembezoni mwa jamii au katika matukio ya majanga makubwa.

- Uteuzi huu unaanza mara moja tarehe 01 Juni 2025. Itakumbukwa kwamba, Monsinyo Romanus Mbena alipadrishwa kunako mwaka 1992 Jimbo Katoliki Morogoro na mwaka 1995 akajiunga na huduma ya Diplomasia ya Kanisa. Tangu wakati huo amehudumu kwenye Balozi za Vatican nchini Zambia, Panama, Ghana Trinidad na Tabago, Sudan, Ethiopia, India na Albania.
 


Baba Mtakatifu Leo XIV amemteuwa Monsinyori Romanus Mbena kuwa ni Mkuu wa Ofisi ya Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo, ambaye hadi kuteuliwa kwake amekuwa akihudumu kama Afisa Mshauri wa Balozi za Vatican ngazi ya kwanza na Mhudumu katika masuala ya jumla kwenye Sekretarieti kuu ya Vatican. Monsinyori Romanus Mbena alipadrishwa mwaka 1992 Jimbo Katoliki la Morogoro na kuanza utume wake katika Diplomasia mwaka 1995.
  • Baraza hili liko chini ya Mtunzaji mkuu wa Sadaka ya Kipapa anayeshirikiana na Mabaraza mengine, ili kuhakikisha kwamba, misaada inawafikia walengwa, kutoka kwa Khalifa wa Mtakatifu Petro, Mchungaji mkuu wa Kanisa la Kiulimwengu kwa ajili ya maskini, watu wanaosukumiziwa pembezoni mwa jamii au katika matukio ya majanga makubwa.

  • Uteuzi huu unaanza mara moja tarehe 01 Juni 2025. Itakumbukwa kwamba, Monsinyo Romanus Mbena alipadrishwa kunako mwaka 1992 Jimbo Katoliki Morogoro na mwaka 1995 akajiunga na huduma ya Diplomasia ya Kanisa. Tangu wakati huo amehudumu kwenye Balozi za Vatican nchini Zambia, Panama, Ghana Trinidad na Tabago, Sudan, Ethiopia, India na Albania.
 
Sawa, hongera zake,tunaomba azidishe upendo asipandishe mabega
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…