Papa Leo XIV kufanyiwa upasuaji kuondoa uvimbe kwenye pafu

Strong ladg

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
1,357
Reaction score
3,114
Pope_Leo_XIV_web_banner_01.jpg

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV, ametangaza kuwa atafanyiwa upsasuaji ndani ya siku chache zijazo ili kuondoa uvimbe kwenye mojawapo ya mapafu yake..

Papa Leo alitangaza hayo siku ya jumapili ya tarehe 11 Oktoba 2026.

Papa Leo alisema kuwa madaktari wamegundua uwepo wa uvimbe ulio kwenye hatua za awali sana na ambao haujasambaa hivyo kwa kufuata ushauri wa madaktari ,atafanyiwa upasuaji ili kuuondoa.

Soma Pia: Pope Leo XIV agunduliwa kuwa na cancer ya pafu

Ameomba sala za waumini wakati akielekea kufanya upasuaji huo.
 
Huu ni mwanzo wa kifo chake, uvimbe mapafuni?! Ni hatari endapo operesheni itashindwa
 
Huyo ndiye kiongozi wa dini, siyo wale watawala haramu ambao huwa wanaficha maatizo yao ya kiafya.

Mungu mkuu, tunaomba ukuu na upendo wako ukapate kuonekana, ukamjalie afya njema mtumishi wako aliyeyatoa maisha yako kwaajili ya kukutumikia.
 
Wazungu mtu ana uvimbe mdogo kwenye mapafu, wala hajalazwa wala hana homa kwamba ameshindwa kufanya kazi ila wamegundua.

Huku Lukuledi mtu kama huyo anajiona mzima wa afya. Kazi kupondea vyakula vya Ulaya eti vina sumu wakati wenzetu life expectancy ni kubwa sana kutuzidi.
 
Huu ni mwanzo wa kifo chake, uvimbe mapafuni?! Ni hatari endapo operesheni itashindwa
Labda kama huo upasuaji umefanyika Amana au Mwananyamala lakini kama ni ulaya kama kufa atakufa kwa sababu siku zimefika siyo kwa sababu ya upasuaji wa uvimbe kwenye mapafu.
 
Uzuri wa RC wao wanaamini kwenye kazi na sala,elimu nasala,mapambano na sala hawaamini miujiza tu na tena miujiza yao wanayoiamini ni ile inayokuja baada ya jitiada (kanisa linazungukwa na shule na hospital)
 
Wazungu mtu ana uvimbe mdogo kwenye mapafu, wala hajalazwa wala hana homa kwamba ameshindwa kufanya kazi ila wamegundua.

Huku Lukuledi mtu kama huyo anajiona mzima wa afya. Kazi kupondea vyakula vya Ulaya eti vina sumu wakati wenzetu life expectancy ni kubwa sana kutuzidi.
Mkuu, huyo ana madaktari wake na alikuwa anafanya checkup kawaida ndo akakutwa na hiyo shida. Hapa kwetu tunasubiri tuumwe ndo tukaonane na madaktari,wao hawasubiri. Sasa angekuwa Bongo asingegundulika mapema bali angegundulika muda umeenda ambapo imefikia stage mbaya ya kufa.Pengine hata angekufa ghafla bila chanzo kujulikana
 
Ulikumbuke kanisa lako lililoenea popote duniani ulikamilishe katika upendo pamoja.
 
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV, ametangaza kuwa atafanyiwa upsasuaji ndani ya siku chache zijazo ili kuondoa uvimbe kwenye mojawapo ya mapafu yake..
Papa Leo alitangaza hayo siku ya jumapili ya tarehe 11 Oktoba 2026.
Papa Leo alisema kuwa madaktari wamegundua uwepo wa uvimbe ulio kwenye hatua za awali sana na ambao haujasambaa hivyo kwa kufuata ushauri wa madaktari ,atafanyiwa upasuaji ili kuuondoa.
Ameomba sala za waumini wakati akielekea kufanya upasuaji huo.

Wamuombee tu miujiza ya YESU itamsaidia

Mbona wengi wanaombewa tu kwa miujiza

Na Mpaka ngoma wanapona
fasta !!!!
 
Wamuombee tu miujiza ya YESU itamsaidia

Mbona wengi wanaombewa tu kwa miujiza

Na Mpaka ngoma wanapona
fasta !!!!
Kanisa katoliki linajenga hospitali za mabilioni ili mkatibiwe na mkazalishwe uko. Halitegemei miujiza.
 
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV, ametangaza kuwa atafanyiwa upsasuaji ndani ya siku chache zijazo ili kuondoa uvimbe kwenye mojawapo ya mapafu yake..
Papa Leo alitangaza hayo siku ya jumapili ya tarehe 11 Oktoba 2026.
Papa Leo alisema kuwa madaktari wamegundua uwepo wa uvimbe ulio kwenye hatua za awali sana na ambao haujasambaa hivyo kwa kufuata ushauri wa madaktari ,atafanyiwa upasuaji ili kuuondoa.
Ameomba sala za waumini wakati akielekea kufanya upasuaji huo.
Wale waliomtembelea tokea upande huu hawakufanya yao kweli!!
 
Back
Top Bottom