Papa: Messi is better than Pele and Maradona" Ronaldo out of the list again

Papa: Messi is better than Pele and Maradona" Ronaldo out of the list again

Lazima ampigie debe sababu ni muArgentina mwenzake.


Na hapa utasemaje mkuu! Na hawa pia ni waArgentina?
BAADHI YA KAULI ZA WANASOKA KUHUSU LIONEL MESSI

Arsene Wenger {Kocha, Arsenal} – “Ni nani Mchezaji bora wa dunia? LeoMessi. Ni nani Mchezaji bora ambaye hajawahi kutokea? Leo Messi”

Diego Maradona {Mchezaji na Kocha wa zamani wa Argentina} – “Hatimaye nimemuona Mchezaji ambaye atarithi nafasi yangu kwenye nchi ya Argentina na jina lake ni Messi. Messi ana kipaji na anaweza kuwa Mchezaji bora”

Pele {Mchezaji wa zamani wa Brazil} – “Kwa kipindi hiki, Messi ni bora”

nadhani pele unamjua vizuri! leo atamsifia messi kesho atamponda na kumfananisha na vitu vya kijinga, in-short haeleweki.....huyu jamaa moyoni anajua kuwa messi ndie baba wa soka duniani ila hataki kudhihirisha ukweli kwa aibu!

Eidur Gudjohnsen {Mchezaji wa zamani wa Chelsea na Barcelona} – “Control ya Messi ni bora zaidi sijapata kuona. Kiukweli amejaliwa pumzi”

Rafael van der Vaart {Mchezaji wa zamani wa Tottenham} – “Mchezaji bora wa kuwahi kukutana nae? nazani ni Messi. Alitumaliza kabisa”

Klaas jan Huntelaar {Schalke 04} – “Ni nani zaidi, Messi au Cristiano Ronaldo? Messi. Ronaldo ni bora, lakini Messi ni mara kumi zaidi yake”

Sergio Aguero {Mchezaji wa Man City} – “Messi kawa mchezaji bora mara kibao na bado anaendelea kuwania, atakuwa mchezaji bora mpaka astaafu soka”

Antonio Cassano {Mchezaji wa zamani wa Ac Milan} – “Messi ni Mchezaji bora kabisa katika historia ya soka, ndio maana naipenda Barcelona zaidi ya Real Madrid”

Diego Simione {Kocha, Atletico de Madrid} – “Messi peke yake ni hatari zaidi ya Ronaldo, Bale na Benzema kwa pamoja”

Arda Turan {Atletco, Uturuki} – “Messi au Ronaldo mchezaji bora wa dunia? nitasema Ronaldo. Messi ni kutoka sayari nyingine”

Roy Keane {Mchezaji wa zamani wa Man U} – “Wakati nakua nilikuwa shabiki wa Maradona na kwasasa ni shabiki wa zao lake Ronaldo ila Messi ni zaidi sijapatkuona. Najaribu kutafuta mapungufu yake uwanjani lakini nashindwa”

Bacary Sagna {Mchezaji wa Man City} – “Mchezaji bora niliowahi kukutana naye? Messi, akiwa anacheza katika ubora wake. Ni mchezaji bora wa dunia. Soka linaonekana jepesi sana wakati anacheza”

Javier Mascherano {Barcelona} – “Inawezekana sio binadamu, ni vizuri Messi anajitambua yeye ni nani. Messi anacheza zaidi ya kucheza”

Fabio Capello {Kocha wa zamani wa Juventus} – “Katika maisha yangu sijawahi kumuona mchezaji mwenye kiwango, mwonekano na umri ule mdogo, kwakweli anavaa jezi nzito katika moja ya timu kubwa duniani”

Marcello Lippi {Kocha wa zamani wa Italy} – “Bora??? Messi”

Arjen Robben {Bayen Munich} – “Messi ni mchezaji wa sayari nyingine”

Sir Alex Ferguson {Aliyekuwa Kocha wa Man U} – “Wakosoaji siku zote wanauliza wachezaji wa zamani kama Pele wangeweza kucheza mpira wa kileo. Lionel Messi angeweza kucheza miaka ya 50 na sasa kama ambavyo wangefanya Di Stefano, Pele, Maradona, Cruyff kwasababu wote ni
wachezaji wakubwa. Bila ubishi Messi anafiti kote”
_________________________________________________
Mkongwe na aliyewahi kuwa nahodha wa FC Barcelona Carles Puyol anasema kuwa Messi ndiye mwanasoka bora zaidi kuwahi kutokea duniani.

Puyol anasema Messi ni mchezaji ambaye sio rahisi kwa walinzi kumdhibiti kwenye mazingira ya kawaida pasipo kumfanyia madhambi.

Puyol ambaye amestahafu kusakata kabumbu mwaka 2013, alifanya mahojiano na televisheni moja nchini Hispania, alieleza kisa kilichotokea mwaka 2008 wakati FC Barcelona ikifundishwa na Pep Guardiola.

Anasema ilikuwa siku moja wakati klabu hiyo ikifanya mazoezi, aliweka dhamiri ya kumzuia mshambuliaji huyo kwa namna yoyote.

Hata hivyo anasema kila alipojaribu, alikuwa akishindwa kutokana mchezaji huyo kuwa na kasi. Ndipo alipoamua kutumia ubabe, ambapo Pep alimuita na kumtaka asimuumize Messi.

Puyol anasema hakuwa tayari kumsikia kocha wake, na kumuomba asitishe mazoezi kama anataka Messi asiumie..!

Enzi zake Puyol anafahamika kwa aina ya uchezaji wake wa kibabe, kutumia mabavu huku akitumia utemi wake kuwadhibiti washambuliaji hatari.

Hata hivyo alinyoosha mikono kwa Lionel Messi na ndio maana anaamini kuwa mchezaji huyo ni bora hata zaidi ya Pele na Diego Maradona kutokana na vitu adimu anavyovifanya awapo dimbani.
 
Back
Top Bottom