Papaa Msofe akabiliwa na kesi ya mauaji

Hapa Bongo, Ukiwa na pesa na una connection na wakubwa, sheria haina nafasi kwako....

Tunachokiona hapa ni mchezo wa kuigiza tu....mwisho wa siku tutaambiwa, upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha beyond reasonable doubt na kwa hivyo mahakama imemuona mtuhumiwa hana hatia.


Najua mtawaka sana lakini huo ndiyo ukweli...Kesi ya Zombe na wenzie ni mfano hai.

Huyu bwana atakuwa guilty kama tu ame-cross swords na wakubwa na kwa hiyo waamue kumnyamazisha.
 
???

*Mfanyabiashara maarufu, jijini Dar es Salaam, Marijani Msofe 'Papa Msofe', akiongozwa na Askari Polisi na Magereza kuingia kwenye chumba cha Mahakama ya Kisutu kwa ajili ya kusomewa shitaka la mauaji ya Onesphory Kitoli, mahakamani hapo leo


???

*Mfanyabiashara maarufu, jijini Dar es Salaam, Marijani Msofe 'Papa Msofe', akiongozwa na Askari Polisi na Magereza kuingia kwenye chumba cha Mahakama ya Kisutu kwa ajili ya kusomewa shitaka la mauaji ya Onesphory Kitoli, mahakamani hapo


???

Msofe akiandikishwa jina lake na Polisi
 
Kwa kweli huyu jamaa simjuwi zaidi ya kumsikiliza kwa nyimbo za dansi....

Ana elimu gani jamani?? Na anamiliki biashara gani halali??

Wapo wengi wa dizaini hiyo..

Unamkumbuka Papaa Juma Banatozi....huyo alikuwa jambazi kabisa wa kwenda front akiwa na bunduki..aliuawa kwenye mapambano na polisi morogoro some years ago!
 
Muzamili Katunzi, then JB, Fikiri madinda, papa Mdsofe, Ndama mtoto ya Ng'ombe et al hawa waliwezesha bendi za kibongo zenye mahadhi ya DRC kuingiza chomeza za kutambulishwa wezi... JK alikuwa analijua kundi la hawa wahalifu ambalo liliibuka zama za Mkapa na IGP wake Mahita kwa kutambua uhatari wa hawa watu,JK mwanzoini mwa utawala wake aliagiza kuwaweka chini ya uangalizi baadhi yao akiwemo Alex Masawe wa AM hotels. Alikuwa akiwafahamu vizuri na wengine ni maswahiba wa kwenye " kahawa" wazee wa mujini, wameliza sana watanzania na wageni, ukienda kule Tegeta ndio utajua kazi za hawa watu kwenye umiliki wa ardhi. Wameharibu ofisi za umma ikiwemo wizara ya Ardhi, TRA,polisi nk. Kuna wengine mtu huwezi kuwadhania kwa hadhi zao ila ni hatari wapo na wabunge wakiwemo wengi toka kaskazini na kanda ya ziwa. Mnakumbuka kisa cha mbunge mmoja wa zamani wa CCM ambae alighushi vyeti akafikishwa mahakamani kule Mwanza, huyo nae ni mtoto wa mjini kinoma sana
 
TANZANIA inaserikali sikivu,imesikia kilio chenu na itafanyia kazi baada ya 2015 endeleeni kupiga kura ili tumalizie kiporo kilichobaki
 
Jamani Magazeti yanapewa hela ili yapotoshe ukweli!! Magazeti yanamuandika Marijan Msofe kama mfanyabiashara maarufu na mengine PROMINENT businessman?!! Huku wakijua ukweli. Nimepata taarifa kuna kila jitihada zinafanyika kumsafisha hivyo ndio maana magazeti yanapewa hela kutoa hizi habari wakionyesha ni mfanyabiashara mashuhuri.

Kama hamjui ngojea niwamwagie kwakua kwa bahati nzuri nina access na watu wa msofe wa karibu ambao wananimwagia habari wakidhani ni za kishujaa kumbe zinanichefua ajabu.

Wanasema sasahivi kwakuwa habari zimesambaa wanachojaribu ni kuongea na waandishi wa habari na kuwapa hela ili waandike habari zake kwa mtazamo wa kwamba investor mkubwa "PROMINENT BUSINESSMAN" anaonewa kwa majungu ili mahakama itakapomuachia jamii iwe na huruma nae. Ndio maana unaona magazeti yote yanaandika MFANYABIASHARA MASHUHURI na wengine PROMINENT businessman. Maneno haya hayaandikwi bure, yanachaguliwa kwa ustadi mkubwa na yanalipiwa hela nyingi sana na ushahidi wa mwandishi wa gazeti moja kubwa la kila siku alifanya ujinga wakumpa jamaa risiti (nitaiscan niirushe, inasema tangazo lakini sio tangazo ni habari!)

Ukweli wenyewe ni kwamba Marijani Msofe ni PROMINENT CONMAN anayetumia JESHI LA POLISI na BAADHI YA MAWAZIRI tafadhali angalia nimeandika "baadhi" sio wote na hawa baadhi naweza kuwataja kwakuwa nina USHAHIDI. Wakuu hawa wa polisi and mind you while KOVA na KENYELA ni washiriki wake wakuu na mabesti zake lakini nao wanapokea maagizo kutoka juu.

Sasa ukiwataja hawa jamaa (Polisi na Baadhi ya wakuu Serekalini) wanakuwaga wakali kweli, kwani umeona wapiganaji wetu Bungeni wanapowataja kwenye Bunge wenzao wanavyoamka mara moja kuomba muongozo na kuwatoa wapiganaji wetu nje ya Bunge mpaka udhibitisho utolewe na unapotolewa HAKUNA kinachofanyika!

Sasa mimi nisilete majungu hapa maana huu sio uwanja wa majungu ni uwanja wa GREAT THINKERS and I respect it 100% siwezi kuweka majungu. Ngoja nitoe ushahidi wa hayo niliyoyasema.

Kuna Mama mmoja mjane akiitwa Mama Mlay aliyenyanganywa na huyu huyu Papaa Msofe nyumba ya marehemu Mume wake. Huyu Mama alinyanganywa nyumba yake na Marijani Msofe akitumia nguvu ya Jeshi letu la Polisi na baadae KUVUNJA nyumba ya huyu mama. Habari za magazeti ambayo mengine ninayo yanadhibitisha kwamba Msofe alitumia MAPOLISI kupitia kwa KENYELA kwenda KUMNYANGANYA HUYU MAMA MJANE kiwanja chake kwa kuwatoa watu waliokuwa wamewekwa na huyo mama. Gazeti la The African lilisema Mama huyu alikuwa ameweka walizi wa ICV security. Nadahini hii kambuni wakifuatwa wanaweza kuliongelea vizuri ni nani hasa aliwatoa kwenye lindo la Mama Mjane kama ni Msofe au JESHI LA POLISI.

Sasa inaonyesha mama mwenyewe nae ni mpiganaji maana naona hakukubali akaonekana kwenye viombo tofautitofauti vya habari akilalamika na mama Mmoja mpiganaji akamtetea sana Mama Ananelia Nkya. Mama Nkya mkurugenzi wa TAMWA (I have a lot of respect kwa huyu Mama, hana longolongo!) nadhani atakuwa na udhibitisho mkubwa zaidi maana mpaka kuliongelea na kusisitiza haki itendeke akiwatuhumu JESHI LA POLISI KUMLINDA MSOFE lazima ana ushahidi uliosimama kwamba Tapeli Msofe anafanya kazi na jeshi letu la Polisi.

Baada ya Mama Nkya kuongea, RPC KENYELA alionekana kwenye TV nadahani kesho yake au keshokutwa yake lakini nakumbuka ilikuwa TAARIFA YA HABARI YA SAA MBILI ripota akiwa Ufosaro wa ITV. Hapo alionekana Marijani Msofe "Papa Msofe" the PROMINENT CONMAN akidhibitisha kwamba amemsikia Mama Nnkya akimtuhumu na kwamba nyumba wanayoongelea ni yake na hana kesi yoyote na huyo Mama Mjane mahakama yoyote. KENYELA nae ambaye ndiye aliyetuma polisi kuwaondoa watu wa huyo mama mjane na kumpa kiwanja Papaa Msofe akasema kwamba polisi hawahusiki kwenye kesi ya viwanja na kwamba huyo mama aende mahakamani kwani kiwanja ni cha Msofe.

Baadae tukasikia kwenye ITV ikiripotiwa na Ufosaroo tena kwamba huyu Mama Mjane alienda kwa Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani ambapo waziri wa Mambo ya Ndani alimlazimisha Papaa Msofe amrudishie huyu Mama Mjane Kiwanja chake. Gazeti la Majira lilisema huyu Mama hakulipwa fidia yoyote! Gazeti liliripoti waziri wa mambo ya Ndani NAHODHA aliongea tu na msofe na kumwambia amrudishie. Sasa kama kiongozi mkubwa Serekalini ananegotiate na TAPELI ambaye ametumia Jeshi letu la Polisi kumpora mama Mjane unataka ushahidi gani kwamba Tapeli Msofe hatumii Viongozi wa Juu Serekalini na jeshi letu la Polisi! Hakuna majungu hapa na TAFADHALI MAGAZETI YETU MSIWEKE FEDHA MBELE toeni habari za KWELI TU.

Nina habari nyingi za huyu jamaa lakini turudi kwenye mjadala wa leo. Msofe alipomuua Chasphori habari zilizagaa kila mahali lakini tena ni jeshi letu la Polisi lililokuwa linamlinda wakati wote. Gazeti mmoja linaripoti kwamba Marehemu alishavunjiwa mlango na kuibiwa kabla yakuamua kuhama mwaka 2007. Yeye wakati huo alihisi ni Masawe na Msofe ndio waliopanga hizo njama. Baada ya Mumewe kuuwawa na watu wa Msofe, Mjane wa Chasphori Mama Mary Kituli na marafiki zake wa karibu walihaha kupigania haki itendeke lakini hawakupata msaada. Lakini kama ujuavyo wakati wa Bwana ukufika haki itatendeka tu.

Sasa ngoja tuone watakavyochezesha kwenye magazeti na huko Mahakamani maana Tanzania ingawa kuna viongozi waadilifu lakini hao wachache wanaofanya kazi na Papa Msofe wanalichafua sana Jeshi letu la Polisi na Serekani na nadhani ni Wakati umefika viongozi wetu wa Juu waadilifu kuingilia na Kusema SASA BASI!
 
haya majina yalikua yajitajwa tajwa sana na Ze Comedy katika show zao, mzafali katunzi na wengine hao
 
nawakubari sana wachina,
hawana huu muda wa kubeba wachache na kuumiza wengi,ebu jaribuni kufuatilia kesi ya aliyekuwa kiongozi mkuu wa chama cha kijamaa bwana Bo Xilai
mke wake alijihusiha na mauwaji ya mfanyabiashara wa UK na hii imepelekea bwana Bo Xilai kufukuzwa chamani bila kuonewa aibu na mke wake ameshitakiwa kwa kesi ya mauwaji je Tanzania tunaweza hili?



THE wife of the former Chinese leader at the centre of a political scandal did not deny murder at her one-day trial.

Gu Kailai, wife of disgraced politician Bo Xilai, was accused during the trial of poisoning 41-year-old British businessman Neil Heywood after going to drink with him in the hotel room where he was found dead last November, court official Tang Yigan told journalists.She did not deny murder during her one-day trial, which ended Thursday with no verdict, the court said.Gu's government-appointed lawyer did not challenge the charge, but said she had "made significant contributions by reporting offences by other people" and her cooperation should be taken into account, Mr Tang said.He gave no further details, but state news agency Xinhua reported shortly after the hearing in the eastern city of Hefei that four police officials would go on trial for "covering up" Gu's alleged crimes.All four worked in the southwestern city of Chongqing, where Heywood died, and where Gu's husband Mr Bo was Communist Party secretary until he was sacked in March after the allegations first emerged.
 
Huwezi kusema Msofe na vijinga vyenzake vina hela,kwani utajiri wa mtu unapimwa kwa kuendesha gari zuri lakini ni la uwizi na lina utata kwenye kodi au kuwa na nyumba ambayo umedhulumu au umejenga kwenye kiwanja ulicho dhulumu? ua kutunza hela kwenye taarabu?,Huyo Msofe katika hivyo vijumba vyake mbona ha miliki nyumba Prime areas like MASAKI,ambapo angeishi na wanene like Bakhressa,Mkono,Said wa HomeShopping,Yeye anajibana Mikocheni mvua ikinyesha hakuna tofauti na Sinza.Nyie mna danganyika na Demo life,mnajiona mko inferior.Msofe alisha choka dili zilikataa mwishoni alikuwa ni dalali wa magari.Na yule Said Ntimizi yupo wapi naye?amepigika kama mpira wa makaratasi kajificha Mbweni kuja mjini ni ishu kama ilivyo kuwa kuweka maji kwenye pool yake.Need i say More?????????
 
mwingine alikuwa ANAITWA ELLY RAIS WA MBEZI huyu alikufa na ukimwi . ameambukiza h.i.v wanafunzi wengi sana wa secondary kuanzia na mbezi high school hadi tegeta.
 
Tujiulize marehemu MPAKANJIA alikua na biashara gani mpaka akasifika hivyo?
 
Asante ingawa mi nimetekwa na miziki ya hapa bondeni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…