Pape Osman Sakho

Pape Osman Sakho

kalisheshe

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2020
Posts
2,064
Reaction score
4,056
Wanamwita Mzee wa kunyunyiza a.k.a Sadio Mane wa east Africa.

Mpira unaompa shida KIBU DENIS ndio huohuo SAKHO anauchezea atakavyo.

Kiukweli huyu jamaa anajua ni msaada mkubwa kwa Simba SC kama watampata kocha mzuri anaejua kuwatumia wachezaji

Kushindwa kwa Pablo kuwatumia vyema wachezaji ndio kumeifanya Simba SC ishindwe kutamba msimu huu, Ila kama ni wachezaji wapo wakutosha na timu isiingie kwenye mkenge wa kuacha wachezaji wengi kwani kina SAKHO wapo wengi klabuni.

Acha SAKHO aendelee kutoa burudani kipindi hiki MBAPPE na NEYMAR wakiwa likizo.
 
Hatari sana huyu jamaa

IMG-20220624-WA0001.jpg
 
Wanamwita Mzee wa kunyunyiza a.k.a Sadio mane wa east Africa.

Mpira unaompa shida KIBU DENIS ndio huohuo SAKHO anauchezea atakavyo.

Kiukweli huyu jamaa anajua ni msaada mkubwa kwa Simba SC kama watampata kocha mzuri anaejua kuwatumia wachezaji

Kushindwa kwa Pablo kuwatumia vyema wachezaji ndio kumeifanya Simba SC ishindwe kutamba msimu huu, Ila kama ni wachezaji wapo wakutosha na timu isiingie kwenye mkenge wa kuacha wachezaji wengi kwani kina SAKHO wapo wengi klabuni.

Acha SAKHO aendelee kutoa burudani kipindi hiki MBAPPE na NEYMAR wakiwa likizo.
Sio kweli, angalia timu saivi haikamiwi kama ilivyokuwa kabla ya yanga kutangazwa ubingwa.
Pablo technically alikuwa vizuri, kaichukua timu ikiwa kwenye shape mbaya na kaifikisha robo fainali CAF Confederation (na hatujapigwa 5 safari hii), asibezwe, aheshimiwe!
 
Amecheza dhidi ya Yanga zaidi ya mechi 3! Zote hakuwahi kufurukuta mbele ya mabeki wakatili kama Kibwana Shomari, Juma Shaban, Yannick Bangala, na wengineo wengi.

Hivyo kwangu mimi namchukulia tu kama mchezaji anayecheza na jukwaa.
 
Usisahau pia amecheza na beki wa CAF robo final na akafurukuta so usikariri maisha pimbi wewe
Mayele hajafunga mechi tatu zote za Simba je nae tuseme ni mbaya ? Acha ushamba
 
Usisahau pia amecheza na beki wa CAF robo final na akafurukuta so usikariri maisha pimbi wewe
Mayele hajafunga mechi tatu zote za Simba je nae tuseme ni mbaya ? Acha ushamba
Kulikuwa na sababu ya kuniita pimbi, mshamba, nk! Kwani ukimjibu mtu kwa kujenga hoja unapungukiwa nini?
 
Mchezaji MACHACHARI sana sana, ila sio HATARI. Kama ningekuwa kocha ningemshauri aache kukaa na mpira bila sababu za msingi.

Anajipa kazi mno ambayo haiwezi, anapoteza mipira mno, tuseme ana harakati za pimbi, anafanikiwa mara chache mno.

Sakho ni mchezaji ambaye ameifanya Simba ipoteze point au magoli mengi mno msimu huu, hapigi pasi kwa wakati, hajui kuiposition nk.

Kwangu nampa 4/10 na kama Simba watampata Miqueson kwa mkopo kutoka Al ahly basi huyo Sakho aondolewe haraka sana.
 
Back
Top Bottom