Pape Sakho aomba kuondoka Simba SC

Pape Sakho aomba kuondoka Simba SC

Soloma TV Online

Senior Member
Joined
Jun 26, 2023
Posts
104
Reaction score
291
Mchezaji wa Kimataifa wa Senegal na Timu ya Simba Pape Ousmane Sakho amewasilisha maombi kwenye Uongozi wa timu ya Simba ya kuomba kuondoka ili akatafute changamoto nje ya nchi.

Ousmane Sakho aliyebakiwa na mwaka mmoja wa kuwatumikia Wekundu wa Msimbazi ana OFA nyingi barani Ulaya na zilizowekwa wazi ni za timu mbili za daraja la pili katika Taifa la Ufaransa. Timu hizo ambazo ofa zao ziko mezani kutoka Ufaransa ni pamoja na Grenoble na Stade Malherbe Caen.

Iwapo timu ya Simba watafunika juu ya ombi hilo ni wazi Sakho ataitumikia timu hiyo kwa kipindi kilichosalia kisha ataondoka kama mchezaji huru na Simba kutoambulia chochote.
 
na mwenzake banda sijui ni balehe zinawasumbua au kitugani
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Simba haijawahi kuzuia mchezaji, maadamu amepata timu ni swala la kuweka mzigo. binafsi nilikuwa nashangaa kocha anavyomweka bench. ungewapa credit mwanaspoti kwa kucopy habari yao
 
Kwa nini asiweke tu mzigo kwenye akaunti ya klabu, halafu tuone reaction kutoka kwa mashabiki?
Inategemea na mkataba ulivyoandikwa. Kama mkataba ulikuwa wa kijinga jinga, wachezaji watakuchezea sana, na wataweka sana mzigo kwenye akaunti! 😁😁😁
 
Back
Top Bottom