Pape Sakho, thamani inayoelekea sokoni

Pape Sakho, thamani inayoelekea sokoni

Joined
Oct 16, 2015
Posts
20
Reaction score
56
IMG_0452.jpg

PAPE OUSMANE SAKHO,THAMANI INAYOELEKEA SOKONI .

Hii ni dhahabu iliyotoka ardhini na kupitia kwenye moto ,kazi iliyobaki ni namna ya kuipeleka sokoni ,uwezo kipaji na maalifa ndio vinaleta maana ya kuwa sakho ni dhahabu iliyosafishwa .

Maandalizi ya simba sc na mafanikio ndio ngazi rasmi yakupeleka dhahabu hii kwenye masoko makubwa . Simba wanatakiwa kuanza sasa ,kufikiri ni namna gani wanaweza kupata pesa nyingi mapema kabla ya thamani hii haijashuka sokoni .

Anafurahisha akiwa uwanjani,mwenye mbinu na ufundi wa hali ya juu ,kwa hichi anachokionyesha bila shaka simba ya msimu ujao inatakiwa iundwe kupitia yeye

Sina shaka juu ya ya uwezo wake,umri wake ;mafanikio ya simba msimu ujao yatatokana na mchamgo mkubwa kutoka kwa Sakho .

Hapa ndipo jina la sakho litakapoibuka,ataandikwa na kuimbwa pale msimbazi,kisha ataanza kutolewa macho na mapapa wa soka letu afrika.

Mafanikio ya Simba ,nyuma ya pazia kutakua na jina la sakho ,sioni ni namna gani kama simba wanaweza kumzuia mchezaji huyu ikiwa vilabu vikibwa vikimtaka ,hii ni nafasi pekee Simba wanatakiwa waitumie ili kupiga pesa nyingi.

kwanza ni kuongeza thamani ya mchezaji kwa kumpa mkataba mrefu ulio na vipengele vyenye maslahi ,pili ni kuwa na maandalizi imara yatakayo toa matokeo safi ya kufanya vizuri kimataifa .

Hii inahitaji mikakati imara na kujua thamani ya kile ulichonacho,vilabu vingi vya america ya kusini hutumia mbinu hii kupata pesa …dunia ya saivi wachezaji wenye uwezo na mbinu kama sahko ni wachache sana .

Na ni nadra kuwapata,na unapowapata sio rahisi kuwazuia kuondoka maana vilabu vingi vinahitaji huduma yao,wakati simba wanafurahia kile sahko anachokifanya uwanjani ,wanatakiwa wafikirie ni namna gani wanaweza kupata pesa kupitia kile anachokifanya .

Muda ndio huu..

Imeandikwa na Nasri Kulemba
 
Huyu dogo alisifiwa sana Mapinduzi CUP.

Tukarudi kwenye Ligi, nako hakuonekana tena.

Anakuja kuonekana baada ya Yanga SC Kutawazwa Mabingwa.

VICHEKESHO kwa kweli [emoji23][emoji23]
 
Ni mchezaji mzuri sana sana kwani ni washambuliaji wachache sana (kwa hapa bongo ni yeye na Morison) ambao wana roho ngumu wataona mabeki zaidi ya watatu mbele yao halafu wakaamua sasa naenda na nitapita hapo hapo na kweli akaenda na akapita. Watu wengi nadhani hawataelewa kwanini nasema roho ngumu; ni kwa sababu hebu pata picha mbele yako yupo Yondani na Juma Nyoso tena nje ya 18 halafu unasema napita katikati yao tena kwa chenga za maudhi kama si kutafuta balaa ni zawadi nyingine watakupa hao mabeki katili.

Kikubwa kwa benchi la ufundi wamsaidie abadilike aache ubinafsi acheze kitimu zaidi na si acheze kwa ajili yake binafsi. Na ameshaonyesha pale anapoamua kucheza kitimu zaidi amewasaidia sana Simba.
 
Back
Top Bottom