Nasri A Kulemba
Member
- Oct 16, 2015
- 20
- 56
PAPE OUSMANE SAKHO,THAMANI INAYOELEKEA SOKONI .
Hii ni dhahabu iliyotoka ardhini na kupitia kwenye moto ,kazi iliyobaki ni namna ya kuipeleka sokoni ,uwezo kipaji na maalifa ndio vinaleta maana ya kuwa sakho ni dhahabu iliyosafishwa .
Maandalizi ya simba sc na mafanikio ndio ngazi rasmi yakupeleka dhahabu hii kwenye masoko makubwa . Simba wanatakiwa kuanza sasa ,kufikiri ni namna gani wanaweza kupata pesa nyingi mapema kabla ya thamani hii haijashuka sokoni .
Anafurahisha akiwa uwanjani,mwenye mbinu na ufundi wa hali ya juu ,kwa hichi anachokionyesha bila shaka simba ya msimu ujao inatakiwa iundwe kupitia yeye
Sina shaka juu ya ya uwezo wake,umri wake ;mafanikio ya simba msimu ujao yatatokana na mchamgo mkubwa kutoka kwa Sakho .
Hapa ndipo jina la sakho litakapoibuka,ataandikwa na kuimbwa pale msimbazi,kisha ataanza kutolewa macho na mapapa wa soka letu afrika.
Mafanikio ya Simba ,nyuma ya pazia kutakua na jina la sakho ,sioni ni namna gani kama simba wanaweza kumzuia mchezaji huyu ikiwa vilabu vikibwa vikimtaka ,hii ni nafasi pekee Simba wanatakiwa waitumie ili kupiga pesa nyingi.
kwanza ni kuongeza thamani ya mchezaji kwa kumpa mkataba mrefu ulio na vipengele vyenye maslahi ,pili ni kuwa na maandalizi imara yatakayo toa matokeo safi ya kufanya vizuri kimataifa .
Hii inahitaji mikakati imara na kujua thamani ya kile ulichonacho,vilabu vingi vya america ya kusini hutumia mbinu hii kupata pesa …dunia ya saivi wachezaji wenye uwezo na mbinu kama sahko ni wachache sana .
Na ni nadra kuwapata,na unapowapata sio rahisi kuwazuia kuondoka maana vilabu vingi vinahitaji huduma yao,wakati simba wanafurahia kile sahko anachokifanya uwanjani ,wanatakiwa wafikirie ni namna gani wanaweza kupata pesa kupitia kile anachokifanya .
Muda ndio huu..
Imeandikwa na Nasri Kulemba