Papy Tex: Msanii mwenye sauti ya dhahabu ambaye muda wote alijificha kwenye kivuli cha Pepe Kale

Papy Tex: Msanii mwenye sauti ya dhahabu ambaye muda wote alijificha kwenye kivuli cha Pepe Kale

May Day

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Posts
6,311
Reaction score
9,027
Kwa muda wote akiwa anafanya muziki wake basi ni lazima jina lake litatajwa sambamba na jina Pepe Kale(Empire Bakuba)....hata kama kwenye wimbo husika hutoisikia sauti ya Pepe Kale.

Nilibaki nikijiuliza ni kwa nini Msanii anayeonekana kuwa na kipaji chote hiki hakutaka kusimama kwa miguu yake mwenyewe ili hali aliwazidi wengi kwa sauti yake tamu isiyomchosha anayemsikiliza?

Raia huyu wa Zambia aliyekuwa anafanya shughuli zake za kimuziki nchini Congo ni kwamba hakuwa anajiamini ama? Maana naona alikuwa na nguvu tu sawa na Mwanamuziki kama Oliva Ngoma n.k.

papi taksi 01.jpeg

Huyo jamaa alikua hatari sana
Sikiliza kibao nganda monique, mammie, musique clarification na ibetibi ndio utajua kipaji cha Pappy Tex

Tatizo la jamaa hakua mtu wa makuu yaani yeye ni kuimba basi mambo ya kumanage muziki ilikua ni kazi ya Peppe Kalle. Baada ya kifo cha Kabasele Yampanya siku chache mbele nae akapata ajali mbaya huko Ufaransa kitu kilichomfanya asiendelee kuimba.

Lakini mwishoni mwa miaka ya 90 kulitokea kutokuelewana kati ya Pepe na Pappy na ugomvi wao ulitokana na rapa Bileku 'djuna mumbafu' Mpasi ambaye mwanzoni alikua dancer tu wa Empire Bakuba ambapo baadae kutokana na kipaji chake cha kughani akatokea kupendwa sana na Pepe Kalle kiasi cha kumpa uongozi katika bendi. Jambo hilo lilimuuma sana sana Pappy Tex kwa sababu ndani ya bendi alikua ana nafasi sawa na Pepe ila aliamua tu kumuachia uongozi Pepe ili yeye abaki kuimba.

Kihistoria Pepe Kalle na Pappy Tex walikuwa ni marafiki wakubwa sana na kwa pamoja walianzisha bendi ya Empire Bakuba.
 
Ngoma za jamaa ninazikubali sana.
 
nimewawekea hapo nyimbo tano kali za Papy Tex ambazo kwangu ndio nyimbo ambazo haipiti siku kama sijasikiliza.

1. Musique Clarification
2. Sinitia
3. Bupe
4. Ibetibi
5. Mammie

Huu wimbo wa Bupe alimuimbia mwanamke mmoja wa kitanzania kabila mnyakyusa akiitwa Bupe. Video yake ilirekodiwa live wakati Empire Bakuba walipofanya ziara yao ya kimuziki nchini Tanzania.
 
Attachments

Kuna wimbo mmoja wa Empire Bakuba unaitwa Sinitia utunzi wake Pappy Tex ndani yupo rapa hatari Djuna Mumbaf Bileku Mpasi.
Ngoma zote za Pappy Texi zipo chini ya Empire Bakuba, ndio maana nahoji mbona alikuwa Mkali sana tu angeweza kusimamia gemu peke yake.
 
Alikuwa na sauti nzuri Sana, na majungu pia.
Baada ya kifo cha Peppe Kalle hakutaka kabisa Bileku apewe uongozi na umiliki wa bendi kama Peppe Kalle alivyokuwa ameagiza.
Ukawa mwisho wa Empire Bakuba
Ila kiukweli hapa sio kwamba Pepe alichemsha.....hivi Bileku na Pappy nani alikuwa mkubwa kikazi?...au kwa kuwa Pappy hakuwa na asili ya Congo?.
 
Ngoma zote za Pappy Texi zipo chini ya Empire Bakuba, ndio maana nahoji mbona alikuwa Mkali sana tu angeweza kusimamia gemu peke yake.
Kwa haiba ya Papy Tex siamini kama angeweza kusimama yeye kama yeye, ni mtu mmoja mpole sana ambaye alihitaji kuongozwa. We fikiria Pepe Kalle, Papy Tex na Dilu Dilumona ndio waanzilishi wa Empire Bakuba lakini Papy yeye wala hakushiriki kwenye mambo ya uongozi zaidi ya kuimba tena mwanzoni mwa wimbo au kama wimbo ni rhumba ndio anaimba mpaka mwisho.
 
Back
Top Bottom