Huyo jamaa alikua hatari sana
Sikiliza kibao nganda monique, mammie, musique clarification na ibetibi ndio utajua kipaji cha Pappy Tex
Tatizo la jamaa hakua mtu wa makuu yaani yeye ni kuimba basi mambo ya kumanage muziki ilikua ni kazi ya Peppe Kalle. Baada ya kifo cha Kabasele Yampanya siku chache mbele nae akapata ajali mbaya huko Ufaransa kitu kilichomfanya asiendelee kuimba.
Lakini mwishoni mwa miaka ya 90 kulitokea kutokuelewana kati ya Pepe na Pappy na ugomvi wao ulitokana na rapa Bileku 'djuna mumbafu' Mpasi ambaye mwanzoni alikua dancer tu wa Empire Bakuba ambapo baadae kutokana na kipaji chake cha kughani akatokea kupendwa sana na Pepe Kalle kiasi cha kumpa uongozi katika bendi. Jambo hilo lilimuuma sana sana Pappy Tex kwa sababu ndani ya bendi alikua ana nafasi sawa na Pepe ila aliamua tu kumuachia uongozi Pepe ili yeye abaki kuimba.
Kihistoria Pepe Kalle na Pappy Tex walikuwa ni marafiki wakubwa sana na kwa pamoja walianzisha bendi ya Empire Bakuba.