Ngoma za jamaa ninazikubali sana.Huyo jamaa alikua hatari sana
Sikiliza kibao nganda monique, mammie, musique clarification na ibetibi ndio utajua kipaji cha Pappy Tex
Tatizo la jamaa hakua mtu wa makuu yaani yeye ni kuimba basi mambo ya kumanage muziki ilikua ni kazi ya Peppe Kalle. Baada ya kifo cha Kabasele Yampanya siku chache mbele nae akapata ajali mbaya huko Ufaransa kitu kilichomfanya asiendelee kuimba.
Lakini mwishoni mwa miaka ya 90 kulitokea kutokuelewana kati ya Pepe na Pappy na ugomvi wao ulitokana na rapa Bileku 'djuna mumbafu' Mpasi ambaye mwanzoni alikua dancer tu wa Empire Bakuba ambapo baadae kutokana na kipaji chake cha kughani akatokea kupendwa sana na Pepe Kalle kiasi cha kumpa uongozi katika bendi. Jambo hilo lilimuuma sana sana Pappy Tex kwa sababu ndani ya bendi alikua ana nafasi sawa na Pepe ila aliamua tu kumuachia uongozi Pepe ili yeye abaki kuimba.
Kihistoria Pepe Kalle na Pappy Tex walikuwa ni marafiki wakubwa sana na kwa pamoja walianzisha bendi ya Empire Bakuba.
Ngoma zote za Pappy Texi zipo chini ya Empire Bakuba, ndio maana nahoji mbona alikuwa Mkali sana tu angeweza kusimamia gemu peke yake.Kuna wimbo mmoja wa Empire Bakuba unaitwa Sinitia utunzi wake Pappy Tex ndani yupo rapa hatari Djuna Mumbaf Bileku Mpasi.
Ila kiukweli hapa sio kwamba Pepe alichemsha.....hivi Bileku na Pappy nani alikuwa mkubwa kikazi?...au kwa kuwa Pappy hakuwa na asili ya Congo?.Alikuwa na sauti nzuri Sana, na majungu pia.
Baada ya kifo cha Peppe Kalle hakutaka kabisa Bileku apewe uongozi na umiliki wa bendi kama Peppe Kalle alivyokuwa ameagiza.
Ukawa mwisho wa Empire Bakuba
Kwa haiba ya Papy Tex siamini kama angeweza kusimama yeye kama yeye, ni mtu mmoja mpole sana ambaye alihitaji kuongozwa. We fikiria Pepe Kalle, Papy Tex na Dilu Dilumona ndio waanzilishi wa Empire Bakuba lakini Papy yeye wala hakushiriki kwenye mambo ya uongozi zaidi ya kuimba tena mwanzoni mwa wimbo au kama wimbo ni rhumba ndio anaimba mpaka mwisho.Ngoma zote za Pappy Texi zipo chini ya Empire Bakuba, ndio maana nahoji mbona alikuwa Mkali sana tu angeweza kusimamia gemu peke yake.