Parachichi au korosho?

Gakon

Senior Member
Joined
Apr 21, 2019
Posts
123
Reaction score
855
Habarini wanajamvi bila shaka mko poa kabisa.
Natamani kufahamu zaidi kutoka kwa watu wenye uzoefu wa vilimo vya mazao tajwa hapo juu(parachichi na korosho).wataalamu wa uchumi wa kilimo nisaidieni kufahamu ni lipi zao zuri zaidi kulilima kati ya hayo mawili maana lengo langu ni kufanya kilimo ambacho hakitanihitaji kutumia muda mwingi sana shambani kama vilimo vingine vya bandika bandua.nawasilisha.
 
Vyote ni vilimo vizuri tena vya kimkakati.

Angalia kipato chako kwa sasa,ila kwa kuanza nakushauri kati ya hayo mawili anza korosho kwa maana gharama zake za uendeshaji sio kubwa sana ukilinganisha na parachichi.
 
Umemshauri vizuri kama KWELI anania ya uwekezaji,CHANGAMOTO ya kilimo cha korosho sio sawa na parachichi, maana parachichi inabidi uwe na chanjo cha uhakika cha maji,bila maji hesabu umeumia na mambo mengine kibao,

Sent from my TECNO CC7 using JamiiForums mobile app
 
Vyote ni vilimo vizuri tena vya kimkakati.

Angalia kipato chako kwa sasa,ila kwa kuanza nakushauri kati ya hayo mawili anza korosho kwa maana gharama zake za uendeshaji sio kubwa sana ukilinganisha na parachichi.

Shukrani mkuu maana najipanga nikiwa napata vifaida kidogo niwekeze huko
 
Asante mkuu nadhani sasa nijikite kufuatilia kwa ukaribu kilimo cha korosho.
hivi utaratibu wake wa mauzo hauna changamoto sana?
 
Asante mkuu nadhani sasa nijikite kufuatilia kwa ukaribu kilimo cha korosho.
hivi utaratibu wake wa mauzo hauna changamoto sana?
Cha kukuongezea hapo,ukitaka kulima hayo mazao yafate usilazimishe yakufate,nina maana kwamba kwa mfano korosho ifate kailimie kusini na hiyo parachichi ifate kailimie njombe na maeneo yake ya karibu kwa kufanya hivi utakuwa umeipunguza changamoto ya masoko kwani wafanyabiashara wanafata haya mazao yanapolimwa kwa wingi.
 
Ok sawa kiongozi ipo sahihi,ndio MAANA wakasema kilimo kina tembea

Sent from my TECNO CC7 using JamiiForums mobile app
 
[emoji1420][emoji1420]
 
Vyote ni vilimo vizuri tena vya kimkakati.

Angalia kipato chako kwa sasa,ila kwa kuanza nakushauri kati ya hayo mawili anza korosho kwa maana gharama zake za uendeshaji sio kubwa sana ukilinganisha na parachichi.
Mikorosho gharama yake ipoje ?
 
Mkuu mimi binafsi sijaanza kulima korosho hivyo sina ufahamu nazo kwa sana,ila humu ukitafuta zipo nyuzi zilizoongelea ulimaji wa korosho na zinaweza kukusaidia kukupa mwanga.
Sasa mbona ulisema korosho gharama zake sio kubwa wakati hauna uzoefu nazo?
 
Kilimo bora ni Korosho mkuu,hasa kwa mikoa ya Pwani na kusini mwa Tanzania.
 
Asante mkuu nadhani sasa nijikite kufuatilia kwa ukaribu kilimo cha korosho.
hivi utaratibu wake wa mauzo hauna changamoto sana?
Mkuu kama ni kanda ya kati kwa korosho ni mtihani.kwasababu kipindi cha kipupwe ndo kororsho hutoa maua na upepo huwa mkali hivyo kuangusha maua asilimia kubwaa na kuacha vi maua vichache.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…