Parachichi na uzalishaji wake

Parachichi na uzalishaji wake

Jesusfreak08

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2019
Posts
822
Reaction score
1,803
Habari zenu wadau

Naamini mpo vizuri
Leo tujifunze pamoja kuhusu zao la parachichi

Kila mkulima ambaye anafanya kazi ya kulima na kuvuna lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba anapata mavuno mengi katika kile ambacho anafanya ndio maana kila njia zinatumika kuhakikisha mwishoni kuna kuwa na mavuno ya kutosha.

Kwanza tukiangalia kwenye zao la parachichi kiukweli kuna aina kama tatu za parachichi ambazo zimetofautiana kimuundo pia hata kuzaa nyingine ni ndefu na nyingine nifupi hata pia katika uzaaji wake wa matunda ni tofauti kidogo

Wewe ni shuhuda mzuri katika hili wengi wetu tunafahamu maparachichi ukienda sokoni unaweza kuta utifauti wa muundo, rangi na pia hata ndani pia kuna utofauti kati ya parachichi na parachichi

Katika kusaka kupata mavuno mengi ikagundulika kuna njia ambayo watu hutumia kuhakikisha wanapata mavuno mengi

Njia hii wanapenda kuita sana kubadi lakini kiukweli sio kubadi ni kama tafsida maeneo wanayofanya hili jambo lakini kisayansi ni "Grafting" ambayo inahusika na kuondoa sehemu ya juu ya mche mdogo wa mparachichi na kuweka sehemu nyingine ya mparachichi.

Sasa kinachotokea ile sehemu ya juu ya mmea iliyokatwa huondolewa na kuwekwa sehemu nyingine kutoka kwa aina ya mparachichi unao zaa sana na ule mparachichi hugeuka na kuwa na tabia ya kuzaa sana unapokuwa umekua vizuri

20210916_165514.jpg


Huu ni mfano wa mche ulifanyiwa Grafting basi ukikuwa utakuwa na tabia ya kuzaa sana ijapokuwa mbegu iliyopandwa ni ya kawaida

Na njia hii ni nafuu sana na inapunguza gharama sana sema inahitaji utalaamu na umakini kuifanya bila hivyo si rahisi kufanikiwa kirahisi

20210916_165441.jpg
 
Hivi hizi parachichi zina soko hapa hapa ndani nchini.
 
Back
Top Bottom