Paris, Ufaransa: Hafla ya Ugawaji wa Tuzo ya Ballon d’Or - 2024

Paris, Ufaransa: Hafla ya Ugawaji wa Tuzo ya Ballon d’Or - 2024

ESCORT 1

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2015
Posts
1,412
Reaction score
3,043
Usiku wa leo, kuna hafla ya ugawaji wa tuzo za Ballon dor

Kwa mara ya kwanza tuzo hizo hazitakuwa na majina ya Lionel Messi au Cristiano Ronaldo.

Vinicius Junior wa Real Madrid anatajwa kama mshindi atakayetangazwa hapo baadae.

Sambamba na kutangazwa kwa Mchezaji bora wa Dunia, pia atatangazwa Mchezaji bora wa Dunia wa Kike.

Tuzo nyingine ni kama vile;

Kopa Trophy - Mchezaji Bora chini ya miaka 21

Yashin Trophy - Golikipa Bora wa Mwaka

Gerd Muller Trophy - Mfungaji Bora wa Mwaka

Socrates Award - Tuzo hii inaenda kwa mchezaji anayejishughulisha na shughuli za kijamii

Timu Bora ya Wanaume ya Mwaka

Timu Bora ya Wanawake ya Mwaka

Kocha Bora wa Mwaka

Kocha Bora wa Kike wa Mwaka

Tuzo hizo zitakuwa mubashara kuanzia saa 4:00 usiku kwa Masaa ya Afrika Mashariki kupitia DStv
 
baadhi ya nyota mbalimbali wanaingia ndani ya ukumbi
 
wachezaji wa Man City wanaingia ukumbini

Kabla ya hapo wachezaji wa Barcelona walitangulia akiwemo Lamine Yamal
 
Kama Rodri atabeba tuzo, hatimae dunia ya soka inaenda kutambua mchango wa viungo wa ulinzi
 
Yamal
IMG_4098.jpeg
 
mie naenda na Rodri....hamna mizengwe, matarajio mara nyingi huleta huzuni. Rodri kwa misimu miwili kakiwasha sana. Sema tofauti ni mwamba Rodri ni kiungo na Vini ni mshambuliaji.
Mara nyingi washambuliaji ndio wanaibuka juu kupewa tuzo haswa kwa sababu ya kufunga.
Mabeki na viungo ni wachache sana waliopata hizi tuzo ukilinganisha na washambuliaji.
Rudisheni kumbukumbu nyuma miezi michache iliyopita kwenye euro2024 kule ujerumani mtakumbuka kazi aliyopiga Rodri na Spain National team. Anastahili mazee
 
Back
Top Bottom